loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bilionea Bill Gates abwagana na mkewe Melinda

VYOMBO mbali mbali vya Kimataifa  siku ya leo vinaelezea kuvunjika kwa ndoa  iliyodumu kwa miaka 27 ya  bilionea  mwanzilishi na  mwenyekiti wa programu za kampuni ya  Microsoft, Bill na Melinda Gates.

Katika taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwanukuu wawili hao inasema "hatuamini tena tunaweza kuwa pamoja kama wanandoa, tumejipa nafasi, ila tutaendelea kushirikiana katika biashara zetu.

"Baada ya kufikiria sana na kufanya kazi nyingi juu ya uhusiano wetu, tumefanya uamuzi wa kumaliza ndoa yetu," wawili hao walisema katika ujumbe wao

Walikutana kwa mara ya kwanza miaka ya 1980 wakati Melinda alipojiunga na kampuni ya Bill ya Microsoft.

Bill Gates alifunga ndoa na Melinda French Gates mwaka wa 1994 na wakabarikiwa na watoto watatu, Jennifer, Rory na Fibi.

Aidha wawili hao kwa pamoja ni  waanzilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali likiwemo la Bill na Melinda Gates Foundation ambalo limeweza kuchangia zaidi ya dola bilioni 3.2 kuboresha afya duniani ikiwemo magonjwa ya kuambukiza na  kuhamasisha chanjo kwa watoto.

Pia kupitia shirika hilo liliweza kuchangia dola bilioni 2 kuboresha fursa ya masomo  masomo kwa familia zisizojiweza. Zaidi ya hayo limeweza pia kuchangia dola milioni 477 kwa miradi ya jamii na zaidi ya dola milioni 488 kwa miradi maalum na kampeni mbali mbali za kila mwaka kuhamasisihwa kila mwaka.

Bill Gates ndiye mtu wa nne tajiri zaidi ulimwenguni, kulingana na jarida la Forbes, na ana mali ya thamani ya dola bilioni  124
Alipata pesa kupitia kampuni aliyoianzisha miaka ya 1970, Microsoft, kampuni kubwa ya programu ulimwenguni.

Wawili hao walichapisha taarifa hiyo wakitangaza talaka yao kwenye Twitter.

"Katika kipindi cha miaka 27 iliyopita, tumewalea watoto watatu wa ajabu na kujenga wakfu ambao unafanya kazi ulimwenguni kote kuwezesha watu wote kuishi maisha yenye afya, yenye tija," ujumbe huo ulisema

"Tunaendelea kuwa na imani ya pamoja katika lengo hilo na tutaendelea kufanya kazi pamoja kwenye wakfu wetu , lakini hatuamini tena tunaweza kuwa pamoja kama wanandoa katika sehemu inayofuata ya maisha yetu.

"Tunaomba nafasi na faragha kwa familia yetu tunapoanza maisha haya mapya."

Walikutanaje ?
Melinda alijiunga na Microsoft kama msimamizi wa bidhaa mnamo 1987, na hao wawili walikaa pamoja kwenye dhifa ya chakula cha jioni cha biashara mwaka huo huko New York.

Walianza kuchumbiana, lakini kama Bill alivyokiambia kipindi kimoja cha Netflix: "Tulijaliana sana na kulikuwa na uwezekano wa mawili kutokea : ama, tungeachana au tungeoana."

Melinda alisema alimpata Bill  akiwa mtu wa kawaida inaonekana hata katika maswala ya moyo akiandika orodha kwenye ubao mweupe na "faida na hasara za kuoa".

Walioana mnamo 1994 katika kisiwa cha Lanai cha Hawaii,wakikiripotiwa kukodi helikopta zote za eneo hilo kuwazuia wageni wasiohitajika kupaa na kuja harusini mwao bila kualikwa.

Bill Gates alijiuzulu kutoka bodi ya Microsoft mwaka jana ili kuzingatia shughuli zake za uhisani.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi