loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bashungwa: Tunaendelea kuweka mazingira wezeshi michezoni

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, imesema kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama inaweka mazingira wezeshi ya michezo hapa nchini bila kuwepo kwa vitendo vya rushwa.

Hayo yalibainishwa jana bungeni na Waziri wa Wizara hiyo, Innocent Bashungwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo Rashid Shangazi (CCM).

Katika swali lake la msingi, Shangazi alitaka kujua kwa kiasi gani serikali inakabiliana na kudhibiti vitendo vya rushwa vinavyoonekana kukithiri katika mchezo wa soka hapa nchini.

Bashungwa alisema Wizara yake inapambana na vitendo vya rushwa kwa nguvu zote kwenye michezo na haitaivumilia timu au mshirika yeyote katika michezo atakayetumia rushwa katika kujipatia ushindi.

Awali akijibu swali hilo, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi, alisema serikali inatambua kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika sekta ya michezo hususani mchezo wa soka hali inayoathiri maendeleo ya mchezo huu kwa ujumla lakini pia kuikosesha serikali mapato.

Ndejembi alisema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) imekuwa ikikabiliana na vitendo vya rushwa kwenye mchezo wa soka kwa kufanya uchambuzi wa mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya viingilio katika mechi za mpira wa miguu.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeiagiza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi