loader
Dstv Habarileo  Mobile
Aweso: Miradi chechefu 85 tumepata ufumbuzi

Aweso: Miradi chechefu 85 tumepata ufumbuzi

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza kuipatia ufumbuzi miradi 85 kati ya 177 kwa ghamara ya Sh bilioni 66.9 ambayo ilikuwa ni miradi chechefu.

Akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2021/22 kwa Wizara hiyo, Aweso amesema pamoja na serikali kufanya maboresho ya miundombinu ili kuhakikisha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira vijijini inakuwa bora na endelevu, hali ya huduma  hiyo haikuwa ya kuridhisha kutokana na changamoto za usimamizi na uendeshaji wa miradi ya maji. 

Amesema, "Hali hiyo kwa kiasi kikubwa ilichangiwa na mfumo uliokuwepo, ambapo usimamizi na utekelezaji wa shughuli za Sekta ya Maji ulikuwa kwenye Wizara mbili tofauti ambazo ni Wizara ya Maji na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR- TAMISEMI).
Amesema baada ya hatua ya Rais ya kuhamishwa kwa majukumu ya utoaji wa huduma za maji kutoka OR- TAMISEMI kwenda Wizara ya Maji kumekuwa na mafanikio ya kushughulikia miradi chechefu.

Aweso alisema miradi 177 ilibainika kuwa na changamoto hizo ambapo hadi kufikia mwezi Machi 2021, miradi 85 imepatiwa ufumbuzi na kugharimu Sh bilioni 66.9 na tayari imeanza kutoa huduma ya maji.
 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/d6fc84d609e521596491994eb06ec2e0.jpg

RAIS wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi amesema wakati umefika kwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi