loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mavunde avalia njuga ukarabati wa Barabara

Mavunde avalia njuga ukarabati wa Barabara

MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde, leo ameshiriki na viongozi wa Kata ya Chigongwe kukagua zoezi la kufungua barabara yenye urefu wa kilomita 5.2 kutoka eneo la Chigongwe-Ngh’ambala ikiwa ni sehemu wa utekelezaji wa ahadi za Mbunge huyo za kufungua barabara hiyo ambayo imekuwa kero ya muda mrefu kwa wananchi wa eneo hilo.

Kukamilika kwa barabara hiyo kutapunguza adha ya matumizi ya muda mrefu ya kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo lingine ndani ya kata ambapo awali wananchi walikuwa wakipata tabu kupita maeneo yasiyo rasmi kwa sababu ya kukosekana kwa barabara inayounganisha mitaa husika.

“Tumeanza sasa ukarabati na kuboresha miundombinu ya barabara mbalimbali za ndani ya Jiji na pembezoni ya Jiji ili kuwapunguzia adha wananchi kutokana na kutopitika kwa urahisi kwa baadhi ya barabara katika maeneo mbalimbali.”alisema Mavunde na kuongeza

“Nitendelea kushirikiana na Tarura kuhakikisha tunayafikia maeneo mengi zaidi yenye barabara korofi kadri bajeti itakavyoruhusu”alisema

Naye  Diwani wa Kata ya Chigongwe  Simon Machela amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kutekeleza ahadi hiyo ya ufunguzi wa barabara ambayo itasaidia kuchochea shughuli za maendeleo katika eneo hilo na pia itarahisisha usafiri kwa wananchi hao kutoka eneo moja kwenda nyingine bila usumbufu tofauti na ilivyokuwa awali.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/d4766e607b506cfe8f3676f5ac81bd77.jpg

RAIS wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi amesema wakati umefika kwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi