loader
Dstv Habarileo  Mobile
Bodi ya Mkonge “kuwafua” wakulima wadogo

Bodi ya Mkonge “kuwafua” wakulima wadogo

BODI ya Mkonge Tanzania (TSB) inakusudia kuanza kutoa mafuzo kwa wakulima wa mkonge ili kuongeza uzalishaji wenye tija wa zao hilo ambao bado umeendelea kuwa chini tofauti na mahitaji katika soko la ndani na kimataifa.

Mkurugenzi wa Bodi, Sadi Kambona amesema bodi hiyo itashirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) na Kituo cha Utafiti wa Mkonge na Udongo (TARI – Mlingano).

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa mkonge duniani ikiwa nyuma ya nchi ya Brazil na ikifuatiwa kwa ukaribu na nchi za Kenya na Madagaska. Utafiti unaonyesha kuwa mkulima huzalisha kilo 800 kwa hekta moja, wakati katika nchi zilizo endelea hekta moja inazalisha zaidi ya tani 5.

Kuna zaidi ya wakulima wadogo 7,500 nchi nzima, katika msimu wa kilimo wa 2020/21 wamezalisha kiasi cha tani 11,000 cha nyuzi za mkonge ambazo mkurugenzi wa bodi anakiri ni chache na hazimnufaishi mkulima.

“Tutatoa mafunzo kwa wakulima wa mkonge ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo ili kunufaika kibiashara zaidi,” alisema Kambona. Aliendelea kufafanua kuwa, mkulima hupanda kati ya miche 3,600 na 4,000 kwa hekta moja lakini mavuno ni chini ya tani moja kwa hekta.

Kuna hekta 40,000 ambazo zinategemewa kuvunwa mwaka huu na wataalamu wanakili bado kuna changamoto kuweza kufikia mahitaji ya ndani na nje ya nchi. “Mkakati wetu ni kuongeza uzalishaji wa mkonge hivyo kwa kuliona hilo sisi na wenzetu wa TARI -Mlingano tutashirikiana kutoa elimu kuanzia aina ya udongo,upandaji hadi mavuno," alisema.

Kwa upande mwingine bodi ya mkonge imesema imeanzisha mashamba mapya katika maeneo ambapo mkonge unastawi. Kambona amesema, bodi imesha omba maeneo katika wilaya za Kilindi na Handeni na kugawa kwa wakulima.

Takribani wakulima 2,624 wamenufaika na mpango huo.

Zao la mkonge liliingizwa nchini mwaka 1892 na mtaalamu wa kijerumani Dr. Richard Hindorff ambaye alikuwa ni mtafiti wa mimea na udongo. Mkonge ulisambaa maeneo mengi ya Tanzania bara mpaka kufikia mwanzoni mwa  miaka 1960, Tanzania ilikuwa inaongoza kwa uzalishaji wa mkonge ikifatiwa na Brazil na Mexico kwa mauzo ya tani 230,000 kwa mwaka nje ya nchi. 

Taarifa zinasema Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) imeonyesha nia kuwasaidia wakulima wa mkonge kwa kutoa mkopo wa hadi Shilingi milioni 15.

Kilimo cha mkonge hutumia asilimia 60 ya shamba na hivyo wakulima hushauliwa kutumia asilimia 40 inayobaki kulima mazao mengine kama maharage, kunde, karanga, soya, choroko, alizeti, ufuta, na mahindi ili kuongeza faida.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8a4dda86a0c5e065a2fa794ae5148b4c.jpeg

MKURUGENZI wa Idara ya Diplomasia ya ...

foto
Mwandishi: Na Cheji Bakari, Tanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi