loader
Dstv Habarileo  Mobile
Serikali yatoa masharti kufungua chuo SEKOMU

Serikali yatoa masharti kufungua chuo SEKOMU

SERIKALI inakusudia kukifungua Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) ambacho kilifungwa Novemba 2018 kutokana na viwango duni vilivyobainishwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini, TCU.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amelitaka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kukamilisha taratibu muhimu ambazo serikali iliagiza ili kukifungua chuo hicho. 

Mapema mwaka huu Waziri Mkuu alielekeza Kanisa hilo linalomiliki chuo hicho kukamirisha mahitaji ambayo yataiwezesha tume kukiruhusu chuo kuendelea na udahili. Akizungumza katika hafla ya kuwekwa wakfu na kuingizwa kazini Askofu Mkuu wa Dayosisi hiyo Dkt. Msafiri Mbilu, Waziri Mkuu amesema bado kuna changamoto zinazo hitaji kurekebishwa.

“Nilipata makundi mawili tofauti na kila moja likijipambanua ndio wamiliki wa kanisa hili, niwahakikishieni hili sasa litakwisha na Sekomu itarudi nitaharakisha kupitia kwa haraka kuondoa vikwazo ili chuo kianze kazi,” Waziri Mkuu Majaliwa alisema. “Serikali itatoa muda wa kulipa deni ili Chuo kiendeleze shughuli zake.”

Mbunge wa jimbo la Lushoto, Shabani Shekilindi (CCM) alimwambia Waziri Mkuu kuwa kufungwa kwa chuo hicho kummeathiri wanafunzi kimasomo na uchumi wa Lushoto.

Askofu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Dkt. Msafiri Mbilu, alisema atatoa kipaumbele katika kushughulikia changamoto zinazokikabili chuo hicho ikiwemo kulipa madeni ili kianze kufanya udahili.

Chuo cha Sekomu kilizuiliwa na serikali kufanya udahili mwaka 2018 kutokana na changamoto ikiwemo madeni na baadhi ya walimu kukosa sifa.

Vyuo vingine vilivyo kubwa na kadhia hiyo ni pamoja na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Matibabu na Teknolojia (IMTU), Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mkuu Yakobo (AJUCo).

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/baabeab14b933be107d688386e3d6c90.jpeg

RAIS wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi amesema wakati umefika kwa ...

foto
Mwandishi: Na Cheji Bakari, Lushoto

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi