loader
Dstv Habarileo  Mobile
DPP Mganga, wengine wateuliwa kuwa Majaji

DPP Mganga, wengine wateuliwa kuwa Majaji

RAIS Samia Suluhu, amefanya uteuzi wa majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani 28 ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga, ameteuliwa kuwa Jaji na hivyo nafasi ya DPP kubaki wazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, imesema Rais Samia amefanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufaa saba, amemuongezea muda Jahji wa Mahakama ya Rufani mmoja na ameteuwa Majaji wa Mahakama Kuu 21.

Biswalo Mganga (pichani) aliteuliwa kuwa Mkurugenziwa Mashtaka (DPP) Oktoba 2, 2014 na aliyekuwa Rais wa wakati huo, Jakaya Kikwete nafasi aliyoendelea nayo hadi leo alipotangazwa kuteuliwa kuwa Jaji Mahakama Kuu.

Katika taarifa hiyo Majaji wa Mahakama ya Rufani walioteuliwa ni Patricia Fikirini, kabla ya uteuzi ho alikuwa Jaji Mfawidhi Divisheni ya Biashara, Mahakama Kuu ya Tanzania, Penterine Kente ambaye kala ya uteuzi alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu (Iringa), Dk Faustine Kihwelo ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Lucia Kairo ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Jaji mfawidhi wa Mahakama Kuu (Bukoba), Lilian Mashaka ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Jaji Mfawidhi Divisheni Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Mahakama Kuu (Dar es Salaam), Issa Maige ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Jaji Mfawidhi Divisheni ya Ardhi , Mahakama Kuu (Dar es Salaam) na Abraham Mwampashi ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar. Aidha Rais Samia amemuongezea muda wa miaka miwili Jaji Sivangilwa Mwangesi wa Mahakama ya Rufani kuanzia Februari 15, 2021.

Majaji wakuu wengine walioteuliwa na nafasi zao walizokuwa wakizitumikia awali kwenye mabano ni Katarina Revocatus (Katibu Tawala – Njombe) , Zahara Maruma (Naibu Msajili na Mkuu wa kitengo cha maboresho ya mahakama(JDU), Devota Kamuzora (Naibu Msajili Baraza la Rufani la Kodi – TRAT), Chaba John (Naibu Msajili Mfawidhi), Lilian Itemba ( Wakili wa serikali Mwandamizi ofisi ya Taifa ya Mashtaka),Awamu Mbagwa (Wakili wa Mwandamizi –Ofisi ya Mashtaka Dodoma), Ayoub Mwenda (Mkurugenzi Msaidizi –Ofisi ya Mashtaka ) na Nyigulile Mwaseba (Naibu Msajili Mahakama Kuu – Dar es Salaam).

Wengine ni John Nkwabi (Naibu Msajili- Arusha), Safina Simfukwe (Naibu Msajili – Divisheni ya Ardhi), David Nguyale (Naibu Msajili – Mahakama Kuu, Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi), Frank Habibu (Naibu Msajili Mfawidhi – Mahakama Kuu Mwanza), James Karayemaha (Naibu Msajili – Mahakama Kuu Mwanza), Emmanuel Loitare (Naibu Baraza la Kodi), Abdi Kagomba (Temesa), Arafa Mpinga (Msaidizi wa Katibu Baraza la Mawaziri, Katiba na Sheria, Ofisi ya |Rais Ikulu), Dk Ubena John (Mhadhiri – Chuo Kikuu Mzumbe), Dk Eliamini Laltaika (Mhadhiri Chuo Kikuu Tumaini), Dk Theodora Mwenegoha (Mhadhiri |Chuo Kikuu Dar es |Salaam) na Mwanabaraka Mnyukwa (Mhadhiri Chuo cha Uongozi wa Mahakama).

Aidha taarifa hiyo ya Msigwa inasema uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu umeanza leo Mei 11, 2021 na kwamba tarehe rasmi ya kuapishwa majaji hao itatangazwa badae.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/3fe08270c0704456184a096a8d6fccb5.jpg

RAIS wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi amesema wakati umefika kwa ...

foto
Mwandishi: Na Vicky Kimaro

1 Comments

  • avatar
    Elias H. Lusato
    13/05/2021

    Magazeti ya yatuhabarisha na kutuburudisha habari kemkem za na ndani na nije ya nchi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi