loader
Dstv Habarileo  Mobile
Serikli kuanza kutoa mikopo nafuu kwa wasanii

Serikli kuanza kutoa mikopo nafuu kwa wasanii

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ili kuwasaidia wasanii kupata mitaji kwa kuwapa mikopo ya riba nafuu kuanzia Julai mwaka huu.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Hassan Abbasi, amesema  jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa tamthilika ya ‘We Men’ itakayorushwa na kituo cha Star Times.

“Tayari mfuko huo wa wasanii umepangiwa bajeti yake na kuanzia mwaka huu wa fedha  unaoanza Julai , wasanii mtaweza kunufaika nao ikiwemo kupata mikopo ya kuboresha kazi zenu na kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili.” alisema na kuongeza

“Hivyo ni wakati sasa wa wasanii kuwa karibu na vyama vyenu na taasisi zinazowasimamia wakiwemo Basata, Cosota na Bodi ya filamu, ambao hawa watahusika kwa karibu katika kuratibu suala hili.” alisema.

Katibu huyo amesema kurejesha mfuko huo kutaondoa  malalamiko ya wasanii wengi ambao wanadai wanakuwa na wazo lakini wanashindwa  kuliwazua kutokana na ukosefu wa fedha.

Mfuko huo ulianzishwa Novemba 2019 katika kongamano la Sanaa la Mwalimu Nyerere lililofanyika mkoani Dar es Salaam, ambapo Waziri Mkuu siku hiyo aliuchangia Shilingi milioni tano huku Hayati  John Magufuli aliahidi kuuchangia Shilingi milioni 100 katika uanzishwaji wake.

Aidha alisema serikali imepanga kufanya mapinduzi makubwa katika sanaa na kuwataka wasanii kutengeneza kazi zenye ubora ambazo zitapenya kwenye soko la kimataifa.

“Sio mnatengeneza filamu jambazi anaenda kupora amevua viatu, tumeshatoka huko,” alisema

Katika hatua nyingine Meneja masoko StarTimes, David Malisa, amesema wamejipanga katika kukuza kazi za Sanaa hapa nchini, ambapo kwa mwaka 2020 katika kampuni hiyo jumla ya filamu 104 zimeonyeshwa huku shilingi milioni 280 zikiwa zimewekezwa kwa shughuli hiyo.

Kwa pande wake Max Rioba ambaye ni muandaaji wa tamthilia ya ‘We Men’, alisema wamejitahidi kuiandaa filamu hiyo katika kiwango cha kimataifa na wanaamini italeta mapindusi katika tasnia ya filamu kwa ujumla.

Wasanii waliopo katika filamu hiyo ni pamoja na Max mwenyewe, Wema Sepetu, Shilole, Hemed Suleiman na Grace Mgonjo ambaye ni mke wa Profesa Jay.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/91ce9ae415ca83fa89b96e1bd863ef9d.jpg

RAIS wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi amesema wakati umefika kwa ...

foto
Mwandishi: Na Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi