loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Museveni Aapishwa Kuongoza kwa Muhula  wa Sita

Rais Museveni Aapishwa Kuongoza kwa Muhula wa Sita

 

Yoweri Museveni ameapishwa kuwa Rais wa Uganda kwa muhula wa sita, katika hafla iliyohudhuliwa na viongozi zaidi ya ishirini kutoka mataifa mbalimbali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

“Mimi Yoweri Kaguta Museveni, naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, kwamba nitakuwa mwaminifu kutekeleza majukumu yangu kama Rais wa Uganda, kulinda katiba, na kukuza ustawi wa wananchi wa Uganda… Eh Mwenyezi Mungu nisaidie,” alitamka Rais Museni alieshinda katika uchaguzi uliofanyika mapema mwaka huu.

Bobi Wine, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi - mwanamziki aliyegeuka mwanasiasa, alishika nafasi ya pili kwa kura, kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi nchini humo.

Rais Museveni, mwenye umri wa miaka 76, aliapishwa Mei 12 katika viwanja vya Kilolo huku wageni wakiwa wamevalia barakoa kama njia ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.

Amekuwa madarakani tangu mwaka 1986.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f3e3687b28d5bb159c6d186096610e64.jpeg

MAVUNO ya mahindi katika mwaka huu ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi