loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mtikisiko ma-RC

Mtikisiko ma-RC

RAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa ambao wengi wamebadilishwa vituo isipokuwa wawili walioachwa kwenye vituo vyao.

Aidha wakuu wa wilaya wawili wamepandishwa kuwa wakuu wa mikoa.

Wakati kukiwa na sura mpya zipatazo 10, uteuzi wao umelenga kujaza nafasi za wakuu wa mikoa waliostaafu, aliyemaliza muda wake na mwingine ambaye taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema atapangiwa majukumu mengine.

Katika uteuzi huo, Rais Samia ametimiza kauli aliyoitoa hivi karibuni kuwa serikali itashirikisha watu mbalimbali kwenye uongozi bila kujali vyama, baada ya kumteua Naibu Katibu wa Chama cha ADC, Bara na aliyekuwa mgombea wa urais wa chama hicho uchaguzi wa mwaka 2020, Queen Sendiga kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Walioachwa vituoni Kulingana na taarifa ya Ikulu, wakuu wa mikoa wawili waliobakizwa kwenye vituo vyao ni Thobias Andengenye anayebaki mkoani Kigoma na Marwa Rubirya anayeendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Majukumu mengine Taarifa imesema aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa atapangiwa majukumu mengine na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare amemaliza muda wake.

Saba wastaafu Wakuu wa mikoa ambao wamestaafu na mikoa waliyoongoza kwenye mabano ni Godfrey Zambi (Lindi), Evarist Ndikilo (Pwani), Joachim Wangabo (Rukwa), Rehema Nchimbi (Singida), Idd Kimanta (Arusha), Anna Mghwira (Kilimanjaro), Nicodemus Mwangela (Songwe).

Aliyeteuliwa CCM 

Nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christine Mndeme aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), pia imezibwa kwa Rais kumteua Brigedia Jenerali Wilbert Augustine Ibuge kuwa Mkuu wa Mkoa huo.

14 waendelea Walioendelea na wadhifa lakini kwa kuhamishwa na vituo vipya kwenye mabano ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (Dodoma), Antony Mtaka aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (Lindi), aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel (Mara).

Wakuu wa mikoa wengine walioendelea na wadhifa na mkoa mpya kwenye mabano ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera (Mbeya), aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella (Morogoro), aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti (Mtwara), aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila aliyepangiwa mkoa wa 

Mwanza.

Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge (Pwani), aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti (Rukwa), aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge (Singida), aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Philemon Sengati (Shinyanga), aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (Simiyu), aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Iringa, Ally Hapi (Tabora) na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima amehamishiwa Tanga.

10 wapya Kwa upande wa sura mpya zilizoteuliwa na mikoa waliyopangiwa kwenye mabano ni Omary Mgumba (Songwe), Makongoro Nyerere (Manyara), David Kafulila (Arusha), Amos Makalla (Dar es Salaam), Rosemary Senyamule (Geita), Queen Sendiga (Iringa), Meja Jenerali Charles Mbuge (Kagera), Mwanamvua Mrindoko (Katavi) na Brigedia Jenerali, Wilbert Ibuge (Ruvuma) na aliyekuwa Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Wasifu wateule wapya Mkuu wa Mkoa mteule wa Manyara, Makongoro ni mtoto wa Rais wa Awamu ya Kwanza, Julius Nyerere. Aliwahi kuwa mwanachama wa NCCR-Mageuzi chama alichojiunga nacho mwaka 1995, na kushinda ubunge wa jimbo la Arusha Mjini. Alipoteza nafasi hiyo kutokana na uamuzi wa Mahakama mwaka 1997 na nafasi hiyo kuchukuliwa na Felix Mrema wa CCM.

Alijiunga na CCM mwaka 2000 na mwaka 2004 aliteu-liwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa kuwa Mbunge . Tangu mwaka 2007 hadi 2012, alikuwa Mwenyekiti wa chama mkoa wa Mara kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Queen, aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, ni Naibu Katibu Mkuu wa ADC, Bara, alizaliwa mwaka 1973. Ni mwanaharakati, mfanyabiashara na mwanasiasa. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 aligombea urais kwa tiketi ya chama hicho.

Rosemary Senyamule ambaye amepangiwa mkoa wa Geita, ni Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. Mwanamvua Mrindoko aliyepangiwa Katavi, ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

Kwa upande wa Makala aliyeteuliwa kuongoza Dar es Salaam, alikuwa Mbunge wa Mvomero tangu 2010. Mwaka 2013, alikuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, na Michezo, Naibu Waziri wa Maji na Mweka Hazina wa CCM na kuanzia mwaka 2018, alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

Aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kafulila aliwahi kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Songwe kabla ya kuchukua fomu kugombea ubunge Kigoma Kusini katika uchaguzi mkuu mwaka jana 2020 kwa tiketi ya CCM lakini hakufanikiwa. Aliwahi kuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na NCCR Mageuzi.

Mgumba aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo katika serikali ya awamu ya tano.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/170afaf12d1562e467fbfa2e3e8b063b.png

RAIS wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi amesema wakati umefika kwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi