loader
Dstv Habarileo  Mobile
Uchumi kukua kwa asilimia 5.1

Uchumi kukua kwa asilimia 5.1

UCHUMI wa Rwanda unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.1  mwaka huu baada ya kushuka kwa asilimia 3.4 mwaka jana kutokana na janga la virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa covid-19.

Ukuaji huo unatarajiwa kuongezeka hadi  asilimia 7.0 mwaka 2022 na wastani wa asilimia  7.8  mwaka 2023/24 kutokana na shughuli za  kilimo, viwanda, madini na ujenzi.

Waziri wa Fedha, Richard Tushabe alisema hayo bungeni wakati akiwasilisha rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2021/22.

Alisema Rwanda inapanga kuongeza matumizi katika mwaka wa fedha kuanzia Julai Mosi  kwa  asilimia 10  hadi faranga trilioni 3.807 (sawa na dola za Marekani bilioni 3.82 ). 

Alisema wafadhili watafadhili asilimia  16 ya bajeti hiyo na fedha nyingine zitatokana na mapato ya ushuru na madeni,.

Alisema serikali itakopa faranga bilioni 651.5 katika mashirikia ya kimataifa, huku deni la taifa likielezwa kupanda kwa asilimia 13 kwa sababu ya kukopa kwa lengo la kupambana na athari za covid-19, alisema.

Deni lote la umma nchini lilipanda hadi  asilimia 71 ya Pato la Taifa mwishoni mwa mwaka jana na linakadiriwa kufikia asilimia  79.7 mwishoni mwa mwaka huu.

"Tunakubali kwamba viwango vya deni vimepanda lakini bado hatujafikia kiwango kibaya  cha deni," alisemaTushabe.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8f36ae9db4225b15140d9e9f8786cefa.jpeg

MAVUNO ya mahindi katika mwaka huu ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi