loader
Dstv Habarileo  Mobile
Morocco alia na washambuliaji  wake

Morocco alia na washambuliaji  wake

BAADA ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 nyumbani dhidi ya Tanzania Prisons, Kocha Mkuu wa timu ya Namungo, Hemed Suleiman ‘Morocco’ , amesema kuwa hajafurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na safu yake ya ushambuliaji hivyo amepanga kulifanyia kazi suala hilo.

Namungo wenye pointi 41 wanashika nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, katika michezo 10 mfululizo ya mashindano mbalimbali, timu hiyo imefunga mabao nane na kufungwa mabao saba.

Akizungumza na gazeti hili kocha, Suleiman, alisema kuwa katika michezo minne iliyosalia anapaswa kupata ushindi na atafanikiwa katika hilo iwapo kama washambuliaji wake watatumia kila nafasi watakayopata.

“Tumebakiza michezo minne ya Ligi  ambayo itatoa taswira kama tutapata  nafasi ya kuingia katika nafasi nne za juu katika msimamo na kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho kama tulivyofanya msimu huu,” alisema Morocco.

Namungo imebakiza michezo minne ambapo mchezo ujao itawafuata Biashara United, kisha kurejea nyumbani kuwakabili Azam FC na baadae kuwafuata  Ruvu Shooting na watamaliza michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuwavaa Simba katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

 

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi