loader
Prince Elvis Macoko: Kijana mwenye ndoto ya kuteka biashara ya muziki

Prince Elvis Macoko: Kijana mwenye ndoto ya kuteka biashara ya muziki

MARA kadhaa nimebahatika kuitembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kikazi na nilichogundua kwa mwaka sasa wa kufanya kazi kwa karibu na taasisi hiyo, ni jiko linalopika vipaji vinavyoweza kupeperusha bendera ya Tanzania kimataifa katika nyakati zote.

Katika safari zangu za kikazi chuoni hapo, mbali na kuzungumza na walimu pia nimepata nafasi mara nyingi kuzungumza na wanafunzi wanaochukua kozi mbalimbali ikiwamo za sanaa na utamaduni katika taasisi hiyo.

Wote niliowahi kuzungumza nao, nilikugundua uwezo mkubwa wa kujieleza walionao, nidhamu na ndoto kubwa walizonazo kupitia tasnia ya Sanaa na Utamaduni kama njia muhimu ya kupata ajira na kuitambulisha nchi kimataifa.

Mwishoni mwa wiki hii, nimebahatika kufanya mahojiano na kijana mwenye umri wa miaka 23 mwanafunzi wa TaSUBa ambaye kwa sasa ana tuzo mbili, ikiwamo ya Afrika na zote zikibeba ndoto za maisha yake kuwa mfanyabiashara mkubwa wa muziki wa kimataifa.

Huyu si mwingine bali ni Prince Elvis Macoko, kijana mtanashati, mpole na anayezungumza kwa nukta huku akichambua maneno ya kuongea. Macoko, mtoto wa sita kwa baba na mtoto wa kwanza kwa mama, alizaliwa Juni 5, mwaka 1998 mkoani Arusha katika Hospitali ya Mount Meru. Jana ilikuwa kumbukizi ya kuzaliwa kwake, heri ya siku ya kuzaliwa Prince Macoko.

Akizungumza na HabariLEO, Macoko aliyelelewa zaidi na mama yake anasema pamoja na kuzaliwa Arusha, yeye kwa kabila ni Mpare wa Same Kisiwani mtoto wa sita kwa baba na mtoto wa kwanza kwa mama akiwa na mdogo mmoja kwa upande wa mama.

Amesoma na kumaliza darasa la saba katika Shule ya Msingi St Dorcas, Moshi, Kilimanjaro mwaka 2012 na akajiunga na Shule ya Sekondari ya Wavulana ya St Joachim iliyopo Same, mkoani humo mwaka 2013 na kuhitimu kidato cha nne mwaka 2016. Kidato cha tano na sita alisoma katika Shule ya Sekondari Kigurunyembe, mkoani Morogoro na kuhitimu mwaka 2019.

Safari ya kujiunga na TaSUBa:

Anasema wazazi wake hasa mama Belloh Mkwazu alipenda sana awe mfanyabiashara. Hii inatokana na namna alivyokuwa akifanya vizuri katika masomo ya biashara alipokuwa sekondari na alipenda masomo hayo kutokana na alivyomuona mama yake akifanya biashara na kufanikiwa kuwasomesha yeye na mdogo wake.

Hata hivyo, anasema pamoja na kufanya vizuri katika masomo ya biashara, alipenda zaidi kuwa mwanamuziki wa kimataifa na ndicho kilichomsukuma kujiunga na TaSUBa mara alipohitimu kidato cha sita.

“Kilichonisukuma kuja TaSUBa ni kuanzia darasa la sita nilikuwa nikipenda sana muziki. Nilipofika kidato pili nilipata bahati ya kurekodi wimbo jijini Dar es Salaam unaitwa Nibebe.

“Lakini mbali na huo wimbo, nilikuwa na nyimbo nyingi ambazo sikuzirekodi zilikuwa zinaimbwa na wenzangu na mimi mwenyewe tukialikwa kwenye shule za wasichana kwa kuwa shule yetu ilikuwa wavulana tu. Hapo nilianza kuona kipaji change kinakuwa,” anasema Prince.

Anasema baada ya kuhitimu kidato cha nne, alidhamiria moyoni kuingia kikamilifu kwenye muziki kama ajira na kutaka kupata ujuzi wa darasani ili kuimarisha kipaji chake na kufikia ndoto yake. Hapo ndipo alipotua TaSUBa mara baada ya kuhitimu kidato cha sita.

“Hapa nasoma kozi ya miaka mitatu ya diploma ya Music and Sound Production. Hii inahusika na masuala yote ya muziki, niko mwaka wa pili namaliza mwakani (2022),” anasema Prince aliyekiri kuwa taasisi hiyo inayosimamiwa kwa sasa na Dk Herbert Makoye, inamshika mkono na kumpa ujuzi mkubwa kufikia ndoto zake.

Mkuu wa taasisi hiyo, Dk Makoye anaeleza kumfahamu Macoko na kueleza kuwa tuzo alizopata anastahili na zinampa hamasa yeye na vijana wengine Kamba kazi zao zinaweza kutambulika na wafanye bidii zaidi.

Tuzo:

Kilichonisukuma hasa kumuandikia makala haya kijana huyu, ni namna ambavyo katika umri mdogo, amefanikiwa kupata tuzo mbili, moja ikiwa ya kimataifa. Na jinsi pia anavyotambua mchango wa wazazi wake, wanafunzi wenzake na TaSUBa katika mafanikio yake haya anayoyaelezea kama ni ya awali, kuelekea kuushangaza ulimwengu.

Anamtaja mzazi mwenzake na msanii maarufu nchini Rayvanny ambaye kwake ni dada wa ukoo kuwa ndiye aliyemwelekeza namna ya kushiriki katika mashindano ya kuwania tuzo za muziki za Afrika mwaka huu zilizotolewa Machi, jijini Lusaka nchini Zambia ziitwazo Zikomo Humanitarian Fashion and Music Awards Afrika na kufanikiwa kupata tuzo ya mwanaume bora katika mavazi na muonekano iliyoitwa Best Dressed Male Media Personality in Africa.

“Nilimuona dadangu huyo akiwa ameshiriki hizo tuzo kubwa za Afrika na alikuwa amechaguliwa kwenye vipengele vitatu vya hiyo tuzo nikamwambia kama anaweza kunifanyia mpango nami nikawa ‘nominated’ (nikachaguliwa) kushindania tuzo kwa upande wa wanaume.

“Akanielekeza link, nikafuata maelekezo, nikaingia kwenye akaunti yao kuoamba kuwa ‘nominated’, wakasema nisubiri kuna vitu wanaangalia, wakanitumia email (barua pepe) kuwa wamenichagua kwenye maeneo mawili ambayo ni Best Male Fashionista in Africa na Best Dressed Male Media Personality in Africa,” anaeleza Prince.

Anasema aliwania vipengele hivyo na kura zilikuwa zinapigwa mtandaoni kupitia link waliowatumia mashabiki wake wampigie kura.

“Utakumbuka nilisema tangu sekondari nina watu wengi na marafiki wengi walikuwa wakiimba nyimbo zangu. Wale wale ndio walinipigia kura. Nilikosa kipengele kimoja alichochukua raia wa Uganda, nikapata kimoja cha Best Male Dressed Media Personality in Afrika,” anasema huku 

akimshukuru Mungu kwa hatua aliyofikia.

Hakwenda Zambia kupokea tuzo lakini anawataja wasanii kama Malkia Careen na wana mitindo akiwamo Ria Fernandes kuwa walienda kupokea tuzo wakiwa miongoni mwa washindi wa vipengele mbalimbali. Anasema aliletewa tuzo yake na Ria na kuipokea jijini Dar es Salaam.

Anasema pamoja na kwamba hakwenda, lakini alipokea pongezi kwa kutwaa tuzo hiyo kwa njia ya barua pepe.

Hiyo ni tuzo ya pili kwake, ya kwanza ni ya Chuo Life Award ya Juni mwaka jana (2020) baada ya kuibuka mshindi wa kipengele cha Best Male Artist (Msanii Bora wa Kiume) katika vyuo nchini kwasababu ya uimbaji wake.

Anasema miongoni mwa walioshiriki kumkabidhi tuzo hiyo ni aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Godfrey Mngereza (sasa marehemu) na msanii Steve Nyerere. Anasikitika kwamba mama yake mzazi, Belloh hakufanikiwa kuhudhurua hafla hiyo kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya moyo ya muda mrefu.

“Tuliopata tuzo ile ya Lusaka Zambia, tuliitwa Bungeni, lakini mimi sikwenda kwasabu nauli ilisumbua kidogo,” anaeleza Macoko ambaye zungumza yake inaonesha si mtu wa kuomba omba pesa hata anapokosa huvumilia kutokana na malezi ya kujitegemea na kuridhika na anachopata aliyopewa na mama yake.

Anasema pamoja na kwamba wazazi wake walipenda awe mfanyabiashara mkubwa, mama yake anakiri kuona nyota iking’aa kwa mwanaye. Macoko mwenyewe anasema atahakikisha kiu ya mama yake anaitimiza kwa kuwa mfanyabiashara mkubwa wa muziki.

Macoko anakiri kwamba TaSUBa imeshika na inaendelea kumtia nguvu katika mafunzo. Anasema pia walimpigia kura sana wakati wa tuzo hizo.

“Nina imani kila mtu alishiriki katika suala langu. TaSUBa wamenishika mkono sana katika hizi tuzo. Nimepata cheti cha kutambuliwa na pongezi kutoka chuo, nilikabidhiwa cheti hicho na Mkuu wa Taasisi Dk Makoye na Rais wa Chuo, Richard Mtambo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/537aa40f6c8ecbaee8c0acb35f24ccd8.png

NCHINI Tanzania kuna matajiri wengi wakubwa walioanzia ngazi ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi