loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mbwa watumika kunusa virusi vya corona

Mbwa watumika kunusa virusi vya corona

RWANDA imezindua jaribio la miezi mitatu la kutumia mbwa  maalumu kupima virusi vya Corona kwa kunusa ili kuimarisha juhudi za nchi hiyo kudhibiti kuenea kwa virusi. 

Mbwa watano waliofunzwa kunusa kwa sasa wanatumiwa kugundua virusi kutoka kwa sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa abiria katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kigali.

Kesi hiyo inaungwa mkono na Ujerumani, ambayo imetoa Mfumo wa Mafunzo kwa  Mbwa wa Kugundua vitu mbalimbali (DDTS), na kutoa mafunzo kwa mbwa kutoka Kikosi cha Polisi ya Rwanda.

Katibu wa kwanza wa Ubalozi wa Ujerumani nchini Rwanda Renate Charlotte Lehner,  alisema kuwa walitumia faranga milioni 36  kwa DDTS na mafunzo kwa watunzaji wa mbwa peke yao. 

Mbwa wanaweza kugundua Covid-19  kwa  usahihi karibu na ile ya kipimo cha  PCR kwa dakika moja,PCR ni kipimo cha kitaalamu cha maabara kinachotumika kupima virusi na kutoa matokeo ndani ya saa nane.

Mpango huu unakusudia kupunguza wakati na gharama za kupima Covid-19 kwenye uwanja wa ndege, na kwenye  mikusanyiko ya watu wengi kwa watu kutambua hali zao kwa dakika moja.

"Abiria wanaowasili kwenye uwanja wa ndege hawatagusana na  mbwa wanaonusa , badala yake wataulizwa na kuombwa idhini ya kushiriki katika jaribio hilo  na kutoa sampuli zao ili kupimwa”alisema 

Mkurugenzi Mkuu wa RBC, Dk Sabin Nsanzimana alisema kuwa majadiliano juu ya mradi wa majaribio ulianza mwaka jana na ikiwa awamu ya majaribio itafanikiwa Rwanda itatumia upimaji wa Covid-19  kwa mbwa kwenye uwanja wa ndege.

Nsanzimana alisema idadi ya mbwa wa kunusa kutekeleza zoezi hilo itaongezwa na kuwa takwimu za  awali zinaonyesha kwamba mbwa ni mzuri katika kugundua virusi hivyo kiwango cha ufanisi wa asilimia 94.

Profesa wa masuala ya biandamu katika Chuo kikuu cha Rwanda ,Leon Mutesa, alisema mradi huo kwa mara ya kwanza ulifanyika nchini Ujerumani na kuwa takwimu zilionesha kuwa kumekuwa na matokeo chanya kwa baadhi ya nchi na kuanza kutumia.

Alisema sampuli 7,000 zitatumika katika majaribio hayo,na kuwa inamchukua mbwa dakika tatu kupima sampuli 20 hadi 50 na Rwanda imekuwa nchi ya kwanza Afrika kufanya vipimo hivyo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/bf32abfed935fa11be3054e581b007ff.jpeg

SERIKALI  itatumia takriban  Faranga bilioni 75  kwa miaka ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi