loader
Dstv Habarileo  Mobile
China na mipango yake ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

China na mipango yake ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

KWENYE Mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa uliofanyika Septemba 2020, Rais Xi Jinping aliushangaza dunia kwa kutoa ahadi kuwa China itafikia kilele cha utoaji wa carbon mwaka 2030, na kuanzia hapo itapunguza kiwango hicho hadi kufikia 0 mwaka 2060.

Wataalamu wanakubaliana kuwa China ni moja kati ya nchi tatu zinazochangia utoaji mkubwa wa Carbon duniani, na kutokana na ukubwa wa tatizo hili, kumekuwa na mashaka kuhusu uwezo wa China kutelekeza ahadi iliyotolewa na Rais Xi Jinping.

Lakini tukiangalia mwelekeo wa China katika muongo mmoja na zaidi uliopita, ni wazi kuwa Rais Xi Jinping alipokuwa anatoa ahadi hiyo, alitoa kwa msingi wa kazi inavyoendelea sasa nchini China.

Kwa sasa kikubwa kinachosikika zaidi duniani kuhusu China kwenye suala la mazingira, ni changamoto zake katika kupambana na uchafuzi wa hewa kwa carbon, uchafuzi wa mito na uchafuzi mwingine unaosababishwa na maendeleo ya viwanda.

Lakini hali halisi ni kuwa China haijalikalia kimya tatizo hilo, kuna hatua nyingi za mseto zinachukuliwa na tayari baadhi zimeanza kuwa na matokeo chanya.

Kwanza, tunaweza kuona kuwa muundo wa uchumi wa China umekuwa na mabadiliko. Kwa sasa mkazo wa maendeleo umehamishwa kutoka kwenye kuzingatia ongezeko la kasi la uchumi na kuwa kuzingatia ongezeko bora la uchumi. Kuna wakati mkazo mkubwa uliwekwa kwenye ongezeko la pato la taifa (GDP), na mwamko kuhusu usafi na usalama wa mazingira ulikuwa mdogo.

 

Kuna wakati Rais Xi Jinping wa China alikumbusha watu kuwa milima ya kijani, na mito safi, ni sawa na dhahabu. Alisema hili kusisitiza kuwa ongezeko la uchumi linatakiwa kuzingatia kulinda mazingira ya asili, na sio lipatikane kwa gharama ya uharibifu na uchafuzi wa mazingira.

Ikiwa pia ni kuelekea kwenye lengo hilo, tunaona pia mwelekeo mkubwa wa matumizi ya ndani na hasa sekta ya huduma kuwa injini muhimu ya uchumi, badala ya kutegemea zaidi kusafirisha nje bidhaa ambazo mchakato wa utengenezaji wake huleta madhara. Ndio maana sasa China ina ongezeko kubwa la usafirishaji wa bidhaa za teknolojia ya juu kama vile simu, kompyuta n.k.

Pili, tukiangalia hali ya ndani ya China tunaweza pia kuona mwelekeo mzuri wa matumizi ya nishati endelevu. Kwa sasa katika miji mingi ya China kuna ongezeko kubwa la matumizi ya mabasi ya usafiri wa umma mijini yanayotumia nishati safi kama gesi na umeme. Mbali na usafiri wa umma, hata idadi ya watu binafsi wanaotumia magari yanayotumia nishati ya umeme E-Vehicles na watu wanaotumia pikipiki zinazotumika umeme E-Bikes pia inazidi kuongezeka. Ongezeko hili linatokana na sera mbalimbali za unafuu kwa mfano serikali inatoa ruzuku kwa kampuni zinazotengeneza magari yanayotumia nishati endelevu.

Lakini hata tukiangalia vyanzo vya umeme wa China tunaweza kuona vyanzo vinavyotokana na nishati safi vinaendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka. Kuna mifano kadhaa inayoonesha mwelekeo wa kuendeleza vyanzo vya nishati safi, kama vile shamba kubwa kukusanya nishati ya jua la kama Longyangxia mkoani Tibet na kuzalisha megawati 850 za umeme, na shamba lingine katika kaunti ya Datong. Hadi sasa China ni nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na paneli nyingi za kuvuna nishati ya jua katika kuzalisha umeme.

 

Mwaka 2019 vyanzo vya nishati endelevu ya Umeme nchini China vilitoa asilimia 26 ya umeme wakati kwa Marekani ilikuwa ni asilimia 17, na mwanzoni mwa mwaka 2020, nishati endelevu ilikuwa ni asilimia 40 ya umeme uliounganishwa kwa wakati huo.

 

Tatu, tunatakiwa pia kuangalia mchango wa China katika kuhimiza maendeleo ya matumizi ya nishati endelevu katika sehemu nyingine duniani. Kwa sasa China iko mbele ya nchi zilizoendelea kwenye kuhimiza matumizi ya nishati hiyo, kutokana na kuwa bidhaa zake za kuzalisha au kutumia nishati endelevu ni za bei nafuu, nchi nyingi zinazoendelea zimekuwa zikiagiza vifaa vya kuvuna nishati za jua na upepo. Mwaka 2019 bidhaa za nishati ya jua zilizotengenezwa China ziliuzwa katika nchi na sehemu 200 duniani, na mashine za kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo zinachukua asilimia 41 ya soko la mashine hizo duniani. Kwa sasa pia imekuwa ni jambo la kawaida kuona paneli za kuzalisha umeme wa nishati ya jua hata katika sehemu za vijijini za nchi za Afrika na Amerika Kusini.

Mbali na hatua inazochukua ndani ya nchi, China vilevile inatambua kuwa suala la mazingira ni suala la kimataifa, na tunaona kuwa suala hili ni moja ya vipaumbele kwenye mambo ya kidiplomasia ya China.

Mwezi Aprili mwaka huu Rais Xi Jinping alifanya mazungumzo na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, na Chansela Angela Merkel wa Ujerumani wakijadili namna jinsi China na Umoja wa Ulaya wanavyoweza kushirikiana kwenye kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Katika mwezi huo huo pia, Rais Xi alihutubia mkutano wa baraza la Asia la Boao uliofanyika hapa China, na kusema miradi ya ushirikiano kwenye masuala ya mazingira itakuwa sehemu muhimu ya ushirikiano kwenye pendekezo la “Ukanda mmoja, njia Moja” Belt and Road Initiative.

Licha ya kuwa China bado ina viwango vya juu vya utoaji wa Carbon, ukweli ni kwamba kufanikisha lengo kuanza kupungua kwa viwango hivyo baada ya mwaka 2030 ni suala la muda tu. Utekelezaji endelevu wa sera za kuelekea kwenye matumizi ya nishati endelevu unaonekana wazi. Mwamko katika jamii ya China kuhusu “binadamu kuishi katika hali ya kupatana na mazingira” sasa limejikita hata kwa wachina wa kawaida na sio viongozi tu.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/af07892a7f4242b3baa0ffc054abfcf9.jpeg

TIMU ya taifa ya Tanzania (Taifa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi