loader
Dstv Habarileo  Mobile
Shule zaagizwa kuwa na kibao cha kupimia urefu

Shule zaagizwa kuwa na kibao cha kupimia urefu

SERIKALI imetoa maekekezo kwa Wataalamu wa Lishe kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kuhakikisha kila Shule inakuwa na kibao maalumu cha kupima urefu wa mtoto ili kutambua mwenendo wa makuzi yake.

Hayo yalibainishwa juzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Jenista Mhagama wakati akikabidhi mradi wa Boresha Lishe uliotekekezwa kwa muda wa miaka mitano kuanzia mwaka 2017 hadi 2021.

Mradi huo ulitekelezwa katika mikoa ya Singida na Dodoma kwa Ufadhili wa Umoja wa Nchi za Ulaya, Japan chini ya Usimamizi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).

Waziri Mhagama alisema, lengo la upimaji huo ni kuufuatilia udumavu wa watoto na kubaini lishe wanayoipata majumbani ili kufanya ufuatiliaji.

Alisema mtoto mwenye lishe duni na aliyedumaa watambaini kwa kupitia urefu wake na mkakati huu ni kwa watoto wote waliomaliza muda wa kliniki.

Pia aliiomba Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) na Mamlaka ya Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) kutengeneza vibao vya kupima makuzi ya Watoto kwa kila Mkoa.

Kwa upande wake, Ofisa Lishe Wilaya ya Chamwino, Benadetha Petro alisema mradi wa Boresha Lishe Katika Wilaya ya Chamwino

ulianza kutekekezwa mwaka 2017 ukiwa na lengo la kuboresha lishe na hasa Katika kupunguza udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka miwili.

“Mradi huu ulikuwa na vipengele viwili shughuli zenye muleta matokeo haraka na ya moja kwa moja kwa mlengwa na shughuli zinazolenga Katika kuleta matokeo ya muda mrefu,” alisema.

Alisema kinamama wajawazito, wanaonyonyesha na watoto wenye umri chini ya miaka mitano walipatiwa vyakula lishe, shughuli hizo zilifanyika Katika vituo

vya kutolea huduma 11 kupitia watoa huduma za afya ngazi za vituo na ngazi za jamii waliopewa mafunzo maalumu.

Alisema mradi huo umekuwa na matokeo chanya ambapo mwaka 2018 mradi huo kwa kushirikiana na halmashauri ya Chamwino walifanya utafiti wa awali na kupata takwimu za kwanza za hali ya lishe kwa halmashauri, uzito pungufu (uwiano wa uzito na umri) asilimia 11.4, ukondefu ( uwiano wa uzito na urefu) asilimia 3.4 na udumavu (uwiano wa urefu na umri) asilimia 28.4.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2ac2348df5a76721779dfc0f55f1bdc0.jpeg

RAIS wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi amesema wakati umefika kwa ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi