loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPBL yasaka wadhamini

TPBL yasaka wadhamini

BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPBL) imesema kwa sasa inasaka wadhamini wengine baada ya Kampuni ya Vodacom kutangaza kujitoa.

TPBL wametakiwa kumalizia kiasi cha fedha wanachodaiwa na klabu zinazoshiriki ligi hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mtendaji Mkuu wa TPLB, Almas Kasongo alisema taarifa ya Kampuni ya Vodacom kujitoa Ligi Kuu walikuwa nayo tangu mwaka jana na walishaanza vikao vya ndani na sasa wanatafuta mdhamini mwingine.

Kasongo alidai kampuni hiyo ilishindwa kutimiza makubaliano ya kimkataba ya kutoa Sh bilioni 3 kwa msimu na kuja na mapendekezo ya kutoa Sh milioni 500 na kuahidi fedha iliyobaki sawa na Sh bilioni 2.5 kulipa katika msimu wa 2022/23 wakati mkataba wao unamalizika msimu wa 2021/22.

“TPLB iliwaomba Vodacom kutoa Sh milioni 600 ambayo ni robo ya Sh bilioni 3 za kwenye mkataba na klabu zilikubali mapendekezo hayo, ambayo yalikuwa siri kutokana na siri hiyo kuvuja milango ipo wazi kwa mdhamini mwingine,” alisema Kasongo.

Alisema katika barua yao ya Agosti walisema hawawezi kutimiza yale waliyokubaliana kwenye mkataba, kwani kila msimu walitakiwa kutoa Sh bilioni 3 na katika makubaliano wanadaiwa Sh bilioni 2.5 kutokana na changamoto zinazowakabili na waliwakubalia, 

Kasongo alisema hizo ni fedha za klabu na watakapozilipa watazipeleka kwenye klabu maana walipojulishwa changamoto zinazoikabili kampuni hiyo walikubali kuwavumilia maana kuanzia waanze kudhamini ligi hiyo hawajawahi kukwama.

Awali, Vodacom walisaini mkataba wa miaka mitatu wa udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara wenye thamani ya Sh bilioni 9, ambapo kila mwaka walitakiwa kutoa Sh bilioni 3.

Juni 6, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hisham Hendi alisema imekuwa ni fahari kubwa kwao kudhamini Ligi Kuu Tanzania kwa kipindi cha miaka 10.

Lakini kutokana na mwenendo wa ufanisi wa kampuni hawataendelea. “Tumefurahia ubia na tunapenda, ligi imekuwa ikiitwa jina letu, Lakini kwa kampuni ambayo imetengeneza hasara, leo usipoweza kuinuka juu lazima uangalie gharama zako”.

“Katika mazingira hayo magumu lazima uchukue uamuzi mgumu ,” alisema Hisham.

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi