loader
Dstv Habarileo  Mobile
WAWILI ZAIDI WAJITOSA TFF

WAWILI ZAIDI WAJITOSA TFF

MCHAMBUZI wa masuala ya michezo wa Kituo cha Habari cha Efm, Oscar Oscar amechukua fomu ya kugombea urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) pamoja na Deogratius Mutungi.

Oscar na Mutungi wanaungana na Wallace Karia, Evans Mgeusa na Zahor Haji kuwania nafasi hiyo.

Katika nafasi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochukua fomu ni Lameck Nyambaya, Liston Katabazi na Michael Petro kupitia Kanda namba moja ya mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Morogoro na Pwani.

Wengine ni Khalid Abdallah kupitia Kanda namba mbili ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga na Osuri Kosuri kupitia Kanda namba nne ya mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Dodoma na Singida.

Osuri ambaye ni kocha mwenye leseni B, Nyambaya na Khalid wanatetea nafasi zao kwa kipindi kingine.

Akizungumza na gazeti hili jana Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo alisema hadi saa 10:00 jioni ni wanafamiliana watatu walikuwa wamechukua fomu.

“Waliochukua ni Oscar na Mutungi kwa nafasi ya Mwenyekiti na Osuri, Nyambaya, Khalid, Katabazi na Michael katika nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji. Mwisho wa kuchukua fomu ni Juni 12 saa 10:00 jioni na uchaguzi unatarajiwa kufanyika Agosti 7, jijini Tanga,” alisema Ndimbo.

Alisema fomu za kuwania urais zinatolewa kwa Sh 500,000 na wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanachukua kwa Sh 200,000 na fedha za kuchukulia fomu zinatakiwa kulipwa katika benki ya CRDB tawi la Holland House, namba 01j1019956600, jina la akaunti Tanzania Football Federation na baada ya kufanya malipo unapaswa kuambatanisha risiti yako na fomu.

Karia aliingia madarakani Agosti 12, 2017 katika uchaguzi uliofanyika jijini Dodoma, ambapo alipata kura 95 kati ya kura 127, akifuatiwa na Ally Mayay aliyepata kura tisa sawa Shija Richard.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/6612793424f30b5e60bfa846006d1c12.jpeg

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga inashuka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi