loader
Dstv Habarileo  Mobile
Hisa Milioni 15 zaingia DSE

Hisa Milioni 15 zaingia DSE

HISA milioni 15 zenye thamani ya shilingi bilioni 7.5 za Kampuni ya Kilimo ya JATU PLc zimeanza kuuzwa katika soko la hisa  jijini Dar es Salaam (DSE) kwa lengo la kupanua kilimo nchini.

Kampuni hiyo imeshawanufaisha zaidi ya wanachama 30,000, huku ikiwa na lengo la kuwafikia Watanzania zaidi ya milioni 2.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu  wa JATU, Issa Simbano  alisema ununuzi wa hisa hizo umeanza baada ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kuidhinisha waraka wa matarajio wa kampuni ya JATU PLC kwa ajili ya kuuza hisa milioni 15 kwa Shilingi 500 ulioanza Juni Mosi mpaka Julai 28, mwaka huu.

Uuzaji wa hisa hizo ni kutekeleza majukumu yake chini ya sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (sura ya 79 ya sheria za Tanzania) na Mei 31, mwaka huu iliidhinisha waraka wa matarajio wa kampuni ya JATU PLC kwa ajili ya kuuza kwa umma katika soko la awali.

Alisema kampuni hiyo imeshafanikisha shughuli za kilimo katika maeneo mbalimbali, na kwamba wameshafikia hekari 47,000.

“Mpaka sasa tumeshafikia mikoa 10 na tumefanya kilimo cha machungwa, maparachichi, mahindi, alizeti, mpunga, ndizi na mboga, kwa maeneo yote tuliyozalisha unapata hekari 47,000, tunaamini kupitia kampeni yetu ya buku tano ‘shilingi 500’  inatosha ambayo ni sawa na hisa 10 tutawafikia wananchi wengi zaidi,” alisema

Asema kampuni hiyo imeamua kuingia kwenye soko la hisa ili kupanua kilimo na kuwasaidia wakulima kufanya kilimo chenye tija na kila mwanahisa atalima kulingana na hisa zake.

Alisema JATU PLC pia imepanga kuboresha miundombinu ya kilimo kwa kutoa pembejeo za kisasa za kilimo na mbegu.

Katika kampeni hiyo ya buku tano wasanii mbalimbali akiwemo Tabu Mtingita, MC  Luvanda, Mau Fundi, Piere Liquid na Mwijaku wameteuliwa kuwa mabalozi.

 

 

 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/60771c4f7405219cc68f15705e9ba39a.jpg

HISA milioni 15 zenye thamani ya shilingi ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi