loader
Dstv Habarileo  Mobile
Viwanja vya ndege wanolewa mifumo ya serikali

Viwanja vya ndege wanolewa mifumo ya serikali

MAMENEJA na Wahasibu 58 wa Viwanja vya ndege vya mikoa wameanza mafunzo ya siku nne ya mifumo mbalimbali ya serikali.

Mafunzo hayo yaliyoanza jana kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB3) yanalengo la kuwafanya mameneja na wahasibu kuepuka mianya yote ya matumizi mabaya ya fedha na upotevu wa mapato.

Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Shadrack Chilongani alisema washiriki hao wanafundishwa uandaaji wa bajeti (Plan Rep); namna ya kuandaa mpango kazi na mfumo wa ulipaji serikalini (MUSE).

“Haya mafunzo ni muhimu sana kwa washiriki kwani tumekuwa tukitumia mfumo mwingine ambao kwanza ulihusisha maeneo sita pekee yaani JNIA, Makao Makuu, Mwanza, Arusha, Songwe na Mtwara, ambapo kulisababisha kila wakati wa kuandaa bajeti kuwa-

tumia Wahasibu wa JNIA na Makao Makuu kuingiza taarifa za mwaka za mzima za viwanja kwenye mfumo wa EPICOR 10, lakini sasa baada ya mafunzo kila mmoja atafanya peke yake akiwa kiwanjani kwake kila kitu kitakuwa kikionekana Makao Makuu,” amesema

Chilongani Pia amesema mfumo mpya wa ulipaji serikalini utasaidia kuokoa mamilioni ya fedha yaliyokuwa yakipotea kutokana na kuwalipa watu binafsi waliokuwa na mfumo wa awali wa EPICOR 10, uliokuwa ukitumika katika maeneo machache pekee.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2b701c95785dc0560b0aa835d33a0cb2.png

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi