loader
Dstv Habarileo  Mobile
Shilingi bilioni 2.5 zatumika kuboresha barabara mwanza

Shilingi bilioni 2.5 zatumika kuboresha barabara mwanza

ZAIDI ya Sh bil 2.5 zimetumiwa na Wakala ya Barabara Vijijini na Mjini (TARURA) Jijini Mwanza kujenga na kukarabati sehemu miundombinu katika maeneo tofauti hivyo kuwezesha ubora wa huduma ya usafiri.

Akizungumza na HabariLEO jana Jijini Mwanza, Mhandisi wa TARURA Jijini, Danstan Kishaka alisema katika mwaka wa 2020/21 Jumla ya Sh 2,585,003,742.74 zimetumiwa kujenga na kukarabati miundombinu ya barabra katika maeneo tofauti jijini Mwanza.

Kishaka alisema kuwa kazi zilizofanyika na zinazoendelea kutendeka ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, mawe,changarawe, ujenzi wa mitaro na makalvati, kuzibua mifereji na kuziba viraka vya lami.

Alizitaja kata zilizonufaika na huduma hizo kuwa ni Isamilo, Pamba, Igogo, Butimba, Mkolani, Nyamagana, Mabatini,Kishiri, Lwanhima, Mhandu, Luchelele, Buhongwa,Nyegezi, Mkuyuni na Mahina.

Alisema kazi hizo mpaka sasa zimefikia kiwango cha asilimia 95 kukamilika katika ubora unaotakiwa na TARURA ili ziweze kudumu na hivyo kuliepusha taifa na hasara ya ujenzi wa mara kwa mara.

“Wakati tukiwa karibu kumalizika kwa mwaka 2020/21 ninayo imani kazi zetu hizi zitakuwa zimemalizika hivyo nitowe rai kwa watumiaji wa barabara kuutunza Ili zidumu kwa mda mrefu Ili fedha zinazoekekezwa na serikali katika eneo hilo zitumike katika maeneo mengine”.

Aliyataja makampuni yanayofanya kazi hizo kuwa ni Nyanza Road Works, Good Choice S.M Cleaners, Rock Zone Link, AM & Partners, Rasu, Asa General Supplies and Construction na Soro Engineering Works.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d066e18df24bf126c66b036d1da994b1.jpeg

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Suleiman Shagata, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi