loader
Dstv Habarileo  Mobile
...Ateta na Katibu Mkuu EAC, kuanza ziara Mwanza leo

...Ateta na Katibu Mkuu EAC, kuanza ziara Mwanza leo

RAIS Samia Suluhu Hassan amekutana na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Peter Mathuki na kumtaka kuhakikisha wananchi wanashirikishwa katika masuala mbalimbali yanayofanywa ndani ya Jumuiya.

Amemtaka pia kusimamia vizuri mpango wa kukuza viwanda ndani ya Jumuiya na kuweka mgawanyo mzuri utakaoepusha kuwa na viwanda vya aina moja.

Katika mazungumzo na Mathuki ambaye anakutana na Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo kujitambulisha na kupokea maelekezo ya kazi, alimtaka pia kuimarisha sekta binafsi ambayo ndio inategemewa katika kutatua tatizo la ajira kwa vijana na kukuza uchumi.

Akizungumzia ushirikishaji wananchi, Samia ambaye alimpongeza kwa kushika wadhifa huo na kumtaka kutekeleza majukumu yake kwa juhudi na maarifa, alisema ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki amegusa zaidi ngazi za uongozi na kuwaacha wananchi wakihangaika na vikwazo mbalimbali .

Alitaka Sekretarieti ya Jumuiya hiyo kufanyia kazi changamoto hiyo ushirikiano uonekane hadi katika ngazi ya wananchi.

Alisema ndani ya nchi wanachama wa Jumuiya kuna fursa nyingi ambazo zikitumika vizuri zitasaidia

kukuza uchumi na kuendeleza miundombinu na kuongeza mshikamano.

Dk Mathuki alimshukuru Samia kwa kumpokea na kumpa maelekezo ya maeneo ya kutilia mkazo katika utendaji wake na amemuahidi kuchapa kazi kwa nguvu zake zote kutekeleza maelekezo na matarajio ya marais.

Mathuki aliongozana na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Martin Ngoga, Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki, Jaji Nestory Kayobera na Naibu Katibu Mtendaji, Steven Mlote.

Katika hatua nyingine, leo Rais Samia anaanza ziara ya siku tatu mkoani Mwanza ambako pamoja na mambo mengine, atazindua na kuweka jiwe la msingi kwenye miradi ya maendeleo ya mabilioni ya shilingi iliyoko mkoani humo.

Ziara hiyo inayoanza leo hadi keshokutwa, atafungua kiwanda chenye mtambo wa kusafishia dhahabu na kufungua jengo jipya la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kanda ya Ziwa iliyopo mtaa wa Balewa Nyamagana.

Ratiba inaonesha leo atakagua mradi wa ujenzi wa daraja la JPM- Kigongo-Busisi, atafungua mradi wa maji Misungwi na uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa reli ya kisasa(SGR) katika eneo la Fella wilayani Misungwi. Keshokutwa atazungumza na vijana wa mkoa wa Mwanza katika uwanja wa Mpira wa Nyamagana.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/064856a32d2e1b358cf7cc7c400df0fe.png

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi