loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wamlilia Profesa Baregu

Wamlilia Profesa Baregu

"Pumzika kwa amani Profesa Baregu (Mwesiga). Mmoja wa wasomi walioamini kuwa huwezi kutenganisha taaluma na siasa. Ulitufundisha baadhi yetu tunaokubali msimamo huo wasomi wanaweza kufanya siasa bila kupoteza sifa zao,” ameandika Waziri wa Viwanda na Biashara,  Profesa Kitila Mkumbo kwenye ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Twitter  

Profesa Mwesiga Baregu,  Mwanachama wa Chadema na mwanazuoni, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumapili Juni 13, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Muhimbili, Aminiel Aligaesha  amedhibitisha na kusema, “Amefariki saa tano usiku wa kuamkia leo akiwa ICU (chumba cha uangalizi maalum)  na alikuwa hapo kwa takribani siku 15.”

Mkurugenzi wa Itikadi na Uhusiano wa kimataifa wa Chadema, John Mrema amesema chama kitatoa taarifa rasmi taarifa baada ya kikao na wanafamilia.

"Tunaelekea hospitali ya Muhimbili kukutana na wanafamilia halafu tutatoa taarifa rasmi," amesema Mrema.

Mwingine aliyeandika ujumbe Twitter ni  kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe akimtakia mapumziko mema Profesa Baregu.

Profesa Baregu aliyekuwa mhadhiri wa sayansi ya siasa na utawala wa umma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, baadaye alisitishiwa mkataba wake kwa kile kilichoelezwa kuchanganya utumishi na siasa.

Baadaye alihamia Chuo kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Alikuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chadema hadi mwaka 2019.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/8ae3cf3a7b1f9d42cd67c009a345d954.jpeg

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi