loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Samia awapa neno wafanyabiashara wadogo Mwanza

Rais Samia awapa neno wafanyabiashara wadogo Mwanza

RAIS Samia Suluhu amewataka wafanyabiashara wadogowadogo jijini hapa kutii na kufuata miongozo na sheria inayotolewa na halmashauri ili kuchochea maendeleo yao binafsi na taifa.

Alitoa wito huo leo katika ziara yake ya siku tatu aliposimamisha msafara wake kuzungumza na wananchi wakati akielekea kuzindua jengo jipya la Benki kuu, baada ya ufunguzi wa mtambo wa kuchenjua dhahabu wilayani Ilemela.

Alisema Serikali inatambua changamoto zinazowakumba wajasiriamali wadogowadogo, maarufu kama 'machinga', bodaboda na mama ntilie na  kwamba Serikali inaendelea na mikakati ya kuzitatua kama ilivyoelekezwa kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Nawasihi ndugu zangu, mfuate sheria lakini pia miongozo inayotolewa na viongozi wa halmashauri. Fuateni maelekezo ya wapi mkae, wapi mwende na jinsi ya kufanya biashara zenu. Serikali ipo pamoja nanyi, tutawalinda na kuwasimamia hivyo fuateni sheria," alisistiza.

Alieleza zaidi kwamba serikali imedhamiria kulifanya jiji la Mwanza kuwa kitovu cha biashara kwa nchi zote za maziwa makuu kwa kuondoa changamoto zote za kimaendeleo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/2cbe74a16d274e5b87d19dc489310e82.jpg

POLISI Mkoani Mtwara imikamata watu 15 kwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi