loader
Dstv Habarileo  Mobile
Hatimiliki za Ardhi Dodoma kuanzia Julai Mosi zote kielektroniki

Hatimiliki za Ardhi Dodoma kuanzia Julai Mosi zote kielektroniki

OFISI ya Ardhi mkoa wa Dodoma itaanza kutoa Hatimiliki za Ardhi za Kielektroniki kwa wamiliki wa ardhi kuanzia Julai Mosi, 2021.

Hayo yamebainishwa na Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dodoma, Thadei Kabonga wakati wa utoaji hati za ardhi 223 kwa wananchi waliorasimishiwa maeneo yao kwenye mitaa ya Miganga na Chinyika katika kata ya Mkonze mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.

Kwa mujibu wa Kabonga, kwa sasa ramani zote za mkoa wa Dodoma zipo kwenye mfumo wa kidijitali hivyo ofisi yake itaanza kutoa hati za ardhi za kielektroniki kwa kuwa hati hizo ziko katika nakala laini.

Kwa sasa Wizara ya Ardhi imewekeza, imeboresha na kuongeza matumizi ya mifumo ya kidigitali ambapo tayari Hati za Kielektroniki nchini zimekuwa zikitolewa kwenye manispaa nne za mkoa wa Dar es Salaam ambazo ni Ilala,Temeke, Kinondoni na halmashauri ya manispaa ya ubungo na hati hiyo ni ya kurasa moja.

"Ramani zote za dodoma kwa sasa zipo kidigitali na Julai mosi mwaka huu tunaanza kutoa hati za kieleltroni maana hati zote ziko katika nakala laini," alisema Kabonga. 

Aliwataka wakazi wa Dodoma wanaomiliki ardhi kuhakikisha wanapimiwa maeneo yao na kupata hati kwa kuwa gharama za upatikamaji hati sasa imepungua ukilinganisha na miaka ya nyuma na kusisitiza kuwa lengo la ofisi yake ni wananchi katika jiji la Dodoma kupata hati zao.

Naye Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde aliyekuwa mgeni rasmi kwenye zoezi la kugawa hati kwa wananchi wa mitaa ya Miganga na Chinyika alilielezea tukio la utoaji hati kwa wananchi waliorasimishiwa makazi kuwa ni tukio la kihistoria kwa kuwa hati zinawafuata wananchi katika maeneo yao badala ya wao kuzifuta.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/d6314f58fddd86dbfcfd328361c9bbab.jpg

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi