loader
Dstv Habarileo  Mobile
Madiwani Arusha wataka suluhisho la Wamachinga

Madiwani Arusha wataka suluhisho la Wamachinga

BAZARA la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Arusha limeshauri wataalamu wa halmashauri hiyo kushirikiana kutafuta suluhu ya kuzagaa kwa wamachinga kwenye kila eneo la jiji hilo na kusababisha ukosefu wa mapato kwa baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wenye maduka.

Madiwani hao wakizungumza kwa nyakati tofauti katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya jiji hilo,kikao cha baraza maalum la kujadili changamoto ya biashara holela jiji la Arusha leo, wamesema kabla ya kukutana walichunguza  kiini cha changamoto hiyo na kubaini upotevu mkubwa wa mapato ya halmashauri kutokana na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa kujiita Wamachinga kwa kuhamishia bidhaa zao barabarani na kwenye mitaro ya maji.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Maximilian Iranqhe akizungumza kwa niaba ya Baraza la Madiwani, amesema mapato ya jiji la Arusha kwa kiasi kikubwa yanakwamishwa na  baadhi ya wafanyabiashara wanojifanya Wamachinga na kukataa kukaa katika maeneo ya biashara na badala yake wanapanga bidhaa mbele ya maduka ya wafanyabiashara wenye leseni na  kuwasababishia  kushindwa kulipa kodi.

Iranqhe amewataka wataalam hao kufanya kazi bila kusikiliza siasa  chafu zinazokwamisha maendeleo ya jiji hilo.

“Jiji la Arusha linapaswa kurudisha hadhi yake, watu wasitafsiri vibaya kauli ya marehemu Rais John Magufuli aliyetaka Wamachinga wasibughuziwe,” amesema.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk John Pima amesema uchunguzi wa kina umebaini baadhi ya wafanyabiashara wameacha vizimba vyao katika masoko na kuhamia barabarani na baadhi wameuza  maeneo  yao waliyokuwa wakiyatumia na kwenda kukaa barabarani kwa kisingizio kuwa hawana maeneo ya  kufanyia biashara zao.

Amesema baadhi ya wafanyabiashara wamefunga biashara katika maduka na kujiondoa kwenye mfumo rasmi wa ulipaji kodi, huku wakipanga bidhaa zao barabarani na hivyo kupunguza mapato ya halmashauri.

Dk, Pima ameliambia baraza hilo kuwa, Kamati ya Fedha na Utawala  ya halmashauri hiyo imekutana na wadau wa biashara ikiwamo jumuiya ya wafanyabiashara, jumuiya ya Machinga, viongozi wa masoko, jumuiya ya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji (Akiboa), jumuiya ya wafanyabiashara ya malori na umoja wa madereva na kukubalina mambo ya msingi, ikiwamo wafanyabiashara kuondoa biashara katika mitaro ya maji kupisha usafi.

Amesema wamachinga  wakubali kufuata taratibu za kufanya biashara ikiwa ni kukubali kuhamia katika maeneo maalum yatakayoanishwa  na yanayofaa kwa biashara .

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  Mkoa wa Arusha,  Musa Matoroka amepongeza Baraza hilo  kuendesha kikao kwa ustaarabu na kutoa maamuzi yenye maendeleo,  kwa wananchi wa Jiji la Arusha, kwani  Arusha yenye maendeleo inahitaji umoja na mshikamano katika kufikia malengo yaliyowekwa .

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/595ecfd714970549ac14d393b4472c0d.jpg

POLISI Mkoani Mtwara imikamata watu 15 kwa ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi