loader
Dstv Habarileo  Mobile
Dawati la Jinsia |sekta ya uvuvi lazinduliwa

Dawati la Jinsia |sekta ya uvuvi lazinduliwa

SERIKALI imesema uwepo wa Dawati la Jinsia katika Sekta ya Uvuvi kutasaidia kuimarisha usawa wa kijinsia pamoja na kuboresha uratibu wa serikali hususan uboreshwaji wa Sera ya Taifa ya Uvuvi juu ya mtazamo wa wanawake katika Sekta ya Uvuvi nchini.

Akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dk. Rashid Tamatamah, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo katika Sekta ya Uvuvi,  Amos Machilika,  wakati wa uzinduzi wa dawati hilo jijini Dodoma, amesema wanawake katika sekta ya uvuvi wanachukua nafasi kubwa na muhimu katika mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi.

 Machilika ameongeza kuwa mwezi Novemba mwaka 2019, serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Uvuvi ilisaini makubaliano na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), kutekeleza mradi wa uwezeshaji wa utekelezaji wa mwongozo wa hiari wa kuhakikisha uvuvi mdogo unakuwa endelevu (SSF) katika muktadha wa uhakika wa chakula na kuondoa umasikini.

 Aidha amefafanua kuwa ili kuwaunganisha na kuwatengenezea mazingira mazuri wanawake wote wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi katika Sekta ya Uvuvi nchini, Wizara hiyo  kwa kushirikiana na FAO imeamua kuanzisha Dawati la Jinsia katika Sekta ya Uvuvi kwa ajili ya kutatua kero zinazowahusu wanawake na makundi yaliyo katika mazingira magumu katika Sekta ya Uvuvi na kuzipatia utatuzi.

 Ametaja baadhi ya kero hizo kuwa ni kufanya kazi nzito na kulipwa ujira mdogo au kutolipwa kabisa, unyanyasaji wa kingono, ukosefu wa taarifa juu ya masoko ya bidhaa zao, ukosefu wa elimu juu ya ujasiriamali na usimamizi wa rasilimali fedha.

 Kwa upande wa afisa uvuvi wa Wizara  hiyo, Abdi Hussein,  zoezi la utambuzi wa idadi ya vikundi vya wanawake wanaojihusisha na uvuvi wapatao takriban 6,000 wizara iliunda Jukwaa la Wanawake wanaojihusisha na whughuli za uvuvi nchini (TAWFA) aidha wizara iliona ni vyema kuunda Dawati la Jinsia ili kuwafikia wanawake wote nchini na makundi maalum.

 Naye Katibu Msaidizi wa Jukwaa la Wanawake wanaojihusisha na shughuli za Uvuvi nchini (TAWFA) Fatuma Katula, amebainisha kuwa baadhi ya sheria zimekuwa zikimbana mwanamke, hivyo kupitia Dawati la Jinsia changamoto nyingi zitatatuliwa na lengo ni kufika mbali na kuongeza uchumi wa nchi pamoja na nchi kuona kwamba kinapatikana chakula sahihi na bora.

 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/76eacb836b4d7d49da6f286c97de074e.jpg

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi