loader
Dstv Habarileo  Mobile
TAA YAKABIDHI  VIFAA VYA AFYA  HOSPITALI YA KIVULE

TAA YAKABIDHI  VIFAA VYA AFYA  HOSPITALI YA KIVULE

MAMLAKA  ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imekabidhi vifaa mbalimbali vya afya kwa ajili ya Hospital ya Kivule iliyopo katika wilaya ya Ilala Jijini  Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa TAA katika wiki ya maadhimisho ya Utumishi wa Umma.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Uongozi wa Hospitali leo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Uhusiano wa Mamlaka hiyo, Bi Pamela Mugarula amesema msaada huo umetolewa  ukiwa  na lengo la kumsaidia mama na mtoto.

Amesema, "Kwa kidogo ambacho tulichokipata tumeamua tukitumie kuwavusha hawa wakina mama na watoto wachanga kwani ikumbukwe kuwa Serikali mwaka 2018 ilizindua kampeni ambayo ilikuwa na lengo la kupunguza vifo vilivyotokana na uzazi  na kuhakikisha mama na mtoto wanakuwa salama.

Amesema, "Katika maadhimisho haya ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Mamlaka imeamua kujisogeza karibu na jamii iliyo karibu na viwanja vyetu vya ndege, na ndio maana tukachagua Kivule ambapo kuna hospitali kubwabaada ya kusikia Kivule ina hospitali kubwa hivyo tukaona wanastahili kupata msaada huu ili kupunguza japo kidogo  baadhi ya vifaa watakavyovihitaji  katika hospital hiyo."

Katika maadhimisho hayo ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo uanza tarehe 16 mpaka 23 mwezi Juni kila mwaka,  Mamlaka hiyo ujikita katika kusaidia jamii mbalimbali kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kama; mashuka, barakoa, dawa za kusafishia vyoo, vifaa vya Ofisi, Gloves, Vitakasa mikono, mashine za kuhifadhi vitakasa mikono, mafagio na sabuni za kunawa mikono.

Kiongozi huyo amesema kuwa msaada huu kila mwaka na mwaka huu umelenga kusaidia hospitali haswa katika huduma zinazotolewa kwa mama na mtoto ili waweze  kujikinga na maambukizi mbalimbali na kwamba wataendelea kutoka msaada huo  kadri itakavyowezekana.

Awali akitoa taarifa ya hospitali hiyo Mganga Mfawidhi, Dk Thobias Nyamboto amesema hospitali hiyo inahudumia wakazi wapatao 700,000 wa Manispaa ya Ilala na Wilaya za  jirani za Temeke na Kisarawe.

"Hospitali hii imeanza kutoa huduma Juni 2020 na kwasasa inahudumia wagonjwa wapatao 150 kwa siku ikiwemo wajawazito 50  na tangu kuanza kwa hospitali hii imeweza kuhudumia wagonjwa takribani elfu 24 na wajawazito 708 waliojifungua," alisema Dkt Nyamboto. 

Pia ameeleza  mpaka sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa na wajawazito wanaojifungua kutoka maeneo mbalimbali yaliyo karibu na hospitali hiyo.

Akieleza kuhusu changamoto za hospitali hiyo, Dk Nyamboto alisema hospitali ina changamoto ya kukosekana kwa vifaa tiba mbalimbali vya uchunguzi kama  vile mashine ya mionzi (xray).

Aidha amesema kwasasa wanafanya juhudi kuhakikisha hospitali inaanza ujenzi wa wodi ya wanawake, wanaume na watoto na majengo ya afya ya kinywa na macho.

Naye Muuguzi Mkuu wa Jiji la Dar es Salaam, Gerelada Mumba amesema msaada uliotolewa na TAA  utatumiwa kiusahihi ili kuwahakikisha usalama mama na mtoto dhidi ya maambukizi mbalimbali hivyo wanaamini msaada huu utakuwa endelevu.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/4ac34d23415caf975938bc70749c3fc5.jpg

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi