loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mkurugenzi dawa za kulevya atoa onyo kali

Mkurugenzi dawa za kulevya atoa onyo kali

KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini (DCEA), Gerald Kusaya, ameionya jamii kutoshiriki kwenye biashara ya dawa za kulevya.
Amesisitiza kuwa DCEA iko macho ikifuatilia mambo yote husika kila wakati na kwamba hakuna mtuhumiwa wa biashara hizo atakayeukimbia mkono wa sheria.
Kusaya ameitoa kauli hiyo baada ya kukamata dawa za kulevya kilogramu 88.27, zikiwemo heroin na methamphetamine, eneo la Kimara, jijini Dar es Salaam.
Dawa hizo kwa mujibu wa kamishna huyo, zilikuwa zimefichwa kwenye gari kabla ya kukamatwa na sasa dereva wa gari hilo anashikiliwa na vyombo vya usalama.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/df8f261ad566d8dc58b347aab488a674.jpeg

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi