loader
Dstv Habarileo  Mobile
Gomes aahidi ushindi Simba

Gomes aahidi ushindi Simba

KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Didier Gomes amesema timu yake ipo tayari kwaajili ya kupambana na kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Polisi Tanzania katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa leo.

Akizungumza na gazeti hili juzi wakati wa mazoezi ya timu yake kwenye Uwanja wa Nyamagana, Gomes alisema timu yake ipo katika hali nzuri na hakuna majeruhi.

‘’Tumejipanga vyema na kuhakikisha tunaibuka na ushindi. Tumejiwekea lengo la kuhakikisha mwisho wa  msimu huu tunashinda mataji yote’’ alisema Gomes.

Alisema watacheza mchezo safi na wakuvutia kwa kuhakikisha wanashinda na hawaruhusu bao lolote golini kwao.

Akielezea mikakati zaidi, Gomes alisema kwa msimu ujao atahakikisha anaboresha timu yake na kuhakikisha inafika hatua  ya nusu fainali na kuchukua ubingwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika.

Gomes alisema anawataka wachezaji wake kuhakikisha wanacheza kwa kuiletea timu yao mafanikio na suala la kuhusu wachezaji gani wanabakia na wapi wanaondoka, maamuzi hao atafanya mwisho wa msimu.

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa timu Polisi Tanzania, George Mketo alisema timu yake haijawahi kumfunga Simba katika mchezo wowote, lakini wachezaji wake watapambana na kupata matokeo.

Alisema timu yake itakosa huduma ya mchezaji Mohamed Mmanga, ambaye ni majeruhi. Mketo alisema  lengo lao ni kuhakikisha wanapambana na kumaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 18.

Katika msimamo wa Ligi Kuu, Simba SC ipo kileleni ikiwa na alama 67 baada ya michezo 27, huku Polisi Tanzania wapo nafasi ya nane wakiwa na alama 41 baada ya michezo 30.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9448867cae64f48d76ccaabf35db2e84.jpeg

AISHI Salum Manula sio jina geni ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi