loader
Dstv Habarileo  Mobile
Covid 19 yasababisha uhabaa  wa Mayai – Waziri Ndaki

Covid 19 yasababisha uhabaa wa Mayai – Waziri Ndaki

SERIKALI imesema kuna changamoto ya uzalishaji mayai nchini ambapo yanazalishwa kiasi kidogo kutokana na uhaba wa vifaranga wa kuku wa mayai.

Waziri wa Mifugo  na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema Wizaa yake imefanya uchunguzi Juni 15, 2021 kwenye Miji mikubwa yote nchini na baadhi ya Wilaya ili kujiridhisha juu ya upatikanaji wa mayai, bei ya trei ya mayai na soko lake kwa ujumla.

Alisema uchunguzi huo umebainisha pia tatizo la uhaba wa vifaranga limekuwepo tangu mwaka 2020 kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19 duniani uliopelekea uingizaji nchini wa

vifaranga wa kuku wazazi kupungua  sana hali iliyosababisha  idadi ya kuku wa mayai wanaotaga kwa sasa kuwa wachache na kusababisha kuwepo na uhaba wa mayai nchini.

“Matokeo zaidi ya uchunguzi yanaonesha kwamba bei ya trei la mayai katika ngazi ya mfugaji ni kati ya sh 6,500 mpaka sh 9,000 na vile vile bei ya trei la mayai sokoni ni sh 6,800 katika baadhi ya mikoa mpaka sh 12,000 kwa mikoa ya Katavi,” alisema  na kuongeza

“Bei ya yai moja sokoni au madukani ni kati ya sh 250 mpaka sh 500.”.

Kauli hiyo ya  Waziri Ndaki imekuja kufuatia siku za hivi karibuni kusambaa ujumbe katika mitandao ya kijamii ulioleza uwepo wa mayai mengi nchini kiasi cha kwamba bei yake umeshuka ghafla mpaka kufikia sh 4000 kwa trei.

“Hakuna uwingi wa mayai uliosababisha kushuka kwa bei ya mayai katika ngazi ya mfugaji na sokoni, kinachoonekana zaidi ni kuwa kuna upungufu mkubwa wa mayai nchini uliopelekea bei kupanda bei na  kufikia sh 12,000.

“Taarifa zilizosambazwa ni uzushi mtupu na hazina ukweli wowote, Serikali ilishazuia uingizwaji wa kuku na mazao yake kutokana na uwepo wa tishio la ugonjwa wa Mafua Makali ya Ndege Duniani.”alisema Ndaki

Aidha, Wizara hiyo imekuwa ikitoa vibali maalum vya kuingiza vifaranga na mayai ya kutotolesha ya kuku wazazi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/6b32829798c1fb03e970ee85cf04447c.JPG

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi