loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ndaki: Hakuna Homa ya Nguruwe DSM

Ndaki: Hakuna Homa ya Nguruwe DSM

SERIKALI imewatoa hofu walaji wa nyama ya Ngurume maarufu “Kitimoto’ wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuwa hakuna uwepo wa ugonjwa wa Ngurume katika jiji hilo.

Hayo yamebainishwa na Wizara ya Miguo na Uvuvi baada ya kufanya uchunguzi Juni 6, katika maeneo mbalimbali ya jijini kufuatia hofu iliyozuka baada ya Nguruwe 298 kufa katika mashamba mawili kwa kile kilichodhaniwa ni ugonjwa wa homa ya Nguruwe.

“Baada ya kuchunguza kwa kina kwa wanyama waliokuwa wamebaki kwenye mashamba hayo

pamoja na kuchukua sampuli na kuzipima katika maabara, ilibainika kuwa ilikuwa sio

ugonjwa wa homa ya nguruwe.” alisema Waziri wa Mifungo Mashimba Ndaki

Alisema ufuatiliaji zaidia umefanyika katika maeno yote ya machinjio ya Nguruwe na kuchunguza Nguruwe wanaochinjwa na hapakuwa na viashiria vyovyote vya ugonjwa wa homa hiyo ya Nguruwe.

Ndaki amesema kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wataendelea na  juhudi za kudhibiti kabisa ugonjwa huo nchini.

 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/d4fe95e92ebac17a797c9cf39907add3.jpg

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi