loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mashabiki wa soka 18 Mbaroni, yupo aliyeiba kofia ya Polisi

Mashabiki wa soka 18 Mbaroni, yupo aliyeiba kofia ya Polisi

MASHABIKI  18 wanashikiliwa na jeshi la Polisi kufuatia vurugu zilizozuka wakati wa mechi ya England dhidi ya Scotland ya mashindano ya Euro 2020.

Mechi hiyo ambayo matokeo yalikua sare ya 0- 0, ilichezwa jana kwenye uwanja wa Wembley

Mashabiki hao wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za  kuchochea ubaguzi wa rangi, ulevi na kumshambulia afisa wa Polisi.

‘’Katika doria ya askari inayohusiana na mechi, mashabiki  18 wameshikiliwa na maofisa wa Polisi na wote waliokamatwa ni wanaume’’ alisema mpepelezi na msemaji wa doria,  Joe Stokoe.

Makosa mengine waliokutwa nayo ni umiliki wa madawa ya kulevya na umiliki wa silaha pasipo uhalali.

‘’London imebakia kuwa sehemu hatarishi ya Ulinzi wa Wananchi, kuna miongozo ya kiserikali kila mahali na tunawaomba watu kufuata taratibu hizo na kutokujihusisha kabisa,’’ alisema Stokoe.

Hata hivyo, Afisa huyo wa  polisi  alisema watu wawili walishikiliwa na polisi siku ya Alhamisi usiku, ambapo kijana mwenye umri wa miaka 25 alishikiliwa kwa tuhuma ya udhalilishaji, huku mwingine akishikiliwa kwa tuhuma ya kuiba kofia ya askari.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/570f73eef62cb445afcc5726a4630d20.jpg

AISHI Salum Manula sio jina geni ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi