loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Mwinyi: Fanyeni kazi kwa ukaribu na wananchi

Rais Mwinyi: Fanyeni kazi kwa ukaribu na wananchi

RAIS wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi amesema wakati umefika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya kazi kwa karibu na wananchi waweze kutambua umuhimu wa kuwepo jumuiya hiyo.

Alisema hayo leo  Ikulu, Zanzibar, alipozungumza na ujumbe wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Dk Peter Mathuki, uliofika kwa ajili ya kusalimiana naye.

Dk Mwinyi alisema azma ya Jumuiya hiyo kufanya baadhi ya vikao vyake vya Bunge pamoja na Mahakama Zanzibar, itawafanya wananchi wawe na uelewa wa kuwepo kwake na kujenga imani nayo.

Aidha Rais Mwinyi  alisema upo umuhimu wa kutumia ipasavyo bahari kuimarisha uchumi wa Taifa na kubainisha  Zanzibar kuwa na sera ya Uchumi wa Bluu.  

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Mathuki, alisema hali ndani ya Jumuiya hiyo sasa ni shwari, lengo likiwa ni kuipeleka karibu na wananchi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/7d2c6be9b804524b0afc6a50cf9d2a26.png

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi