loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mtaka, Mavunde waipiga Jeki Jeshi la Polisi

Mtaka, Mavunde waipiga Jeki Jeshi la Polisi

MKUU  wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka,  sambamba na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Anthony Mavunde, wameunga mkono jitihada za wananchi wa Kata ya Chang’ombe za ujenzi wa kituo cha Polisi kwa kuchangia vifaa vya ujenzi na kuahidi kukamilisha ujenzi wa kituo.

Hafla fupi ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo hicho cha Polisi lililowekwa na Mkuu wa Mkoa, Anthony Mtaka, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Katika kukamilisha ujenzi huo wa kituo cha Polisi,Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Waziri wake George Simbachawene wamechangia  sh milioni 10, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kupitia kwa Mkuu wa Mkoa Anthony Mtaka Matofali 6700, yenye thamani ya Sh milioni 10.720.

 Kwa upande wa  Mbunge Mavunde  amechangia  saruji  tani tano pamoja na rangi ya kupaka yenye thamani ya Sh milioni 1.

Akitoa maelezo ya awali,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Ramadhan Kailima,  amesema kituo hicho cha Daraja C kitakuwa ni kati ya vituo vikubwa katika Mkoa wa Dodoma ambacho kitakuwa na uwezo wa kuwa na askari 50 kama watoa huduma na hivyo kupongeza jitihada kubwa za wananchi na viongozi kujiletea maendeleo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/a36a56f157396721dc70b6b255b0924f.jpg

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi