loader
KENNETH KAUNDA Shujaa wa uhamasishaji wa utaifa Afrika na mwanademokrasia mwenye huruma

KENNETH KAUNDA Shujaa wa uhamasishaji wa utaifa Afrika na mwanademokrasia mwenye huruma

KENNETH Kaunda maarufu kama KK, mwanasiasa wa Zambia na Rais wa kwanza wa Zambia kati ya mwaka 1964 hadi 1991, alizaliwa April 28, 1924, Lubwa, karibu na Chinsali.

Kaunda aliyefariki Juni 17, mjini Lusaka, Zambia, ni mwanasiasa aliyeiongoza Zambia kujipatia uhuru mwaka 1964 na kuwa Rais wa kwanza hadi 1991.

Miaka ya awali

Baba yake mzazi kutoka Nyasaland (sasa Malawi), alikuwa mwalimu wa shule, mama yake pia mwalimu alikuwa mwanamke wa kwanza Mwafrika kufundshwa wakati wa ukoloni Zambia.

Wazazi wake wote walifundisha katika eneo la kabila la Bemba, kusini mwa Zambia, ambapo kijana Kaunda alisoma elimu yake ya awali na alihitimu masomo ya sekondari miaka ya 1940.

Kama ilivyokuwa kwa Waafrika wengi kipindi cha ukoloni Zambia, waliosoma middle-class, Kaunda pia alianza kufundisha kwanza enzi za ukoloni Zambia na katikati ya miaka 1940 Tanganyika (ambayo sasa inajulikana kama Tanzania).

Mapambano dhidi ya utawala wa kikoloni

Kaunda alirudi Zambia mwaka 1949. Mwaka huo akawa mkalimani na mshauri wa masuala ya Afrika wa mlowezi huru wa kizungu Stewart Gore-Browne na mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria la Rhodesia Kaskazini.

Kaunda alipata ujuzi wa serikali ya kikoloni na wa kisiasa, vyote ambavyo vilimsaidia baadaye mwaka huo alipojiunga na chama cha African National Congress (ANC), chama cha kwanza Kaskazini mwa Rhodesia (sasa Zambi) kupinga ukoloni.

Mapema miaka ya 1950, Kaunda alikuwa Katibu Mkuu wa ANC, kama ofisa mipango mkuu, nafasi ambayo ilimuweka karibu katika nafasi na maifaili ya harakati. Hivyo, uongozi wa ANC ulipotofau

tiana katika mikakati yake kati ya mwaka 1958–1959, Kaunda alibeba sehemu kubwa ya shughuli za muundo wa ANC na kuuhamishia katika chama kipya kilichojulikana kama Zambia African National Congress.

Kaunda akawa rais wa kwanza wa chama kipya na ujuzi aliokuwa nao, aliutumia kwa ustadi, kughushi sera za wapiganaji dhidi ya mipango ya Waingereza ya Shirikisho la Makoloni ya Rhodesia Kusini(Zimbabwe ), Rhodesia Kaskazini(sasa Zambia) na Nyasaland( sasa Malawi).

Viongozi wa Afrika walipinga na kuhofia shirikisho la namna hiyo, lilikuwa na lengo la kuwapa mamlaka walowezi wachache wa kizungu.

Kaunda aliajiri chama cha Zambia kama chombo cha kutekeleza kile alichoeleza “ hatua nzuri zisizokuwa na vurugu,” mfumo wa kiraia wa kupinga sera ya shirikisho.

Kampeni zake zilikuwa na matokeo makubwa mawili; kwanza serikali ya Uingereza ilibadilisha sera ya shirikisho na mwishowe ilikubali kuitupa, pili kufungwa kwa Kaunda na viongozi wengine wa wapiganaji kuliwainua hadi hadhi ya mashujaa wa kitaifa machoni pa watu.

Kwa hiyo, kuanzia mwaka 1960 kuendelea, uungwaji mkono wa kitaifa wa harakati za uhuru wa Zambia ulipatikana, vile vile nguvu ya Kenneth Kaunda katika harakati hizo.

Kaunda aliachiwa gerezani na serikali ya kikoloni Januari 8, 1960. Mwisho wa mwezi huo alichaguliwa kuwa wa Chama cha United National Independence Party (UNIP), kilichoundwa Oktoba 1959 na Mainza Chona, mpiganaji wa kitaifa.

Chama cha UNIP kilikuwa kwa haraka na kujipatia wanachama 300,000 hadi kufika Juni 1960. Mwezi Desemba 1960, mamlaka za kikoloni za Uingereza zilimualika Kaunda na viongozi wengine wa UNIP kwa ajili ya kushiriki majadiliano ya hali ya makoloni matatu katika mkutano uliofanyika mjini London.

Mapema mwezi uliofuata, serikali ya Uingereza ilitangaza kuanza kuacha kuitawala Zambia rasmi. 

Uchaguzi mkubwa wa kwanza uliomaliza kabisa ukoloni ulifanyika Oktoba 1962. Mapendekezo ya Katiba yaliwapa walowezi wa Ulaya walioko Rhodesia Kaskazini sehemu kubwa ya kura. Hata hivyo vyama vikuu vya Waafrika vya UNIP na ANC vilipata kura nyingi. UNIP kilishinda kwa kupata viti 15 kati ya 37 katika Baraza jipya la kutunga sheria.

Mafanikio ya UNIP yalitokana na uongozi wa Kaunda. Alitumia busara na kuwaondolea hofu waliowezi kuwa utawala wa Kiafrika, utapuuza maslahi yao bila haki na kuzima mgawanyiko miongoni mwa Waafrika mbao ndio walikuwa kwa idadi kubwa nchini humo.

Kwa ujuzi huo huo, Kaunda aliweza kufanya mjadala wa maendeleo zaidi ya Kikatiba na mwaka 1964 Zambia ilipata uhuru na Kaunda kuwa Rais.

Rais wa Zambia

Kama ilivyo kwa viongozi wengine wa Afrika, Kaunda alikabiliwa na matatizo mengi baada ya Uhuru, hasa suala la ukabila.

Alifanikiwa kuendeleza mjadala kwenye suala hilo na kuiokoa Zambia dhidi ya vita ya kikabila. Walakini vurugu za kisiasa ndani ya chama zilitokea wakati wa uchaguzi wa mwaka 1968, ambapo Kaunda na chama chake walirudi madarakani. Mwaka 1972, Kaunda aliweka Sheria ya chama kimoja Zambia na mwaka 1973 alitangaza Katiba mpya ambayo iliidhinisha utawala wa chama kimoja bila kupingwa.

Katika miaka 1970, serikali ya Kaunda ilipata maslahi makubwa katika shughuli za uchimbaji wa madini ya shaba nchini humo na pia ilisimamia vizuri sekta zingine pia, hata hivyo wakati iliweka kiwango kikubwa cha fedha katika sekta ya madini, serikali ilipuuza kilimo na kujikuta ikitumia fedha nyingi kuongeza chakula cha ruzuku kwa masikini waliopo mijini.

Sera hizo zilipunguza uzalishaji wa kilimo na kuongeza utegemezi wa Zambia kuuza shaba nje na kutegemea mikopo na misaada kutoka nje.

Katika masuala ya kigeni, Kaunda aliongoza nchini zingine za kusini mwa Afrika, kukabiliana na serikali za wazungu Rhodesia Kusini (sasa Zimbabwe) na Afrika Kusini. Kaunda alipambania nchi 

zingine, miaka ya 1970, kwa gharama kubwa ya uchumi wa nchi yake na mwishoni mwa miaka ya 1970 aliruhusu Zambia itumike kama msingi kwa ajili ya wapiganani wa msituni wa Kiafrika wakiongozwa na Joshua Nkomo.

Mwaka 1976 Kaunda alichukua madaraka ya dharura na akachaguliwa tena kama rais katika uchaguzi wa mgombea mmoja, mwaka 1978 na 1983. Majaribio kadhaa ya mapinduzi dhidi yake yalifanyika mwanzoni mwa miaka ya 1980, lakini yalishindikana.

Uchumi wa Zambia uliendelea kudorora, kwa sababu ya kushuka kwa bei ya shaba(bidhaa kubwa waliokuwa wakiuza nje), kupanda kwa bei ya mafuta(bidhaa kubwa waliokuwa wanaagiza kutoka nje), kuondolewa kwa misaada ya kigeni na uwekezaji wa nchini zilizoendelea na kukithiri kwa vitendo vya rushwa ndani ya serikali.

Kuongezeka kwa hali ya umma kutoridhika na upinzani wa kisiasa katika hatua za muundo, mwaka 1990 Kaunda alihalalisha vyama vya upinzani na aliweka jukwaa la uchaguzi huru wa vyama vya upinzani katika uchaguzi wa mwaka 1991.

Katika uchaguzi uliofanyika, baadaye mwaka huo, Kaunda na UNIP walishindwa na Chama cha upinzani cha Movement for Multiparty Democracy (MMD). Hivyo mrithi wa Kaunda akawa Frederick Chiluba, aliyechukua madaraka November 2, 1991.

Baada ya Urais

Baada ya kuondoka madarakani, mara kadhaa Kaunda alitofautiana na serikali ya Chiluba na chama chake cha MMD.

Kaunda alipanga kugombea dhidi ya Chiluba katika uchaguzi wa urais mwaka 1996, lakini alikwama baada ya marekebisho ya kikatiba kufanyika na ambayo yalimzuia kugombea.

Desemba 25, 1997, Kaunda alikamatwa na kutuhumiwa kuchochea jaribio la mapinduzi lililotokea mwezi Oktoba mwaka huo. Hata hivyo aliachiwa siku sita baadaye, lakini aliwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani hadi mashtaka yote yalipofutwa Juni 1998.

Mwezi uliofuata Kaunda alitangaza anajiuzulu majukumu na wadhifa wake kama rais wa UNIP, mara atakapochaguliwa atakayemrithi nafasi hiyo. Hata hivyo, ukosefu wa makubaliano juu ya mrithi wake ulisababisha mpasuko ndani ya UNIP na mwishowe 

Kaunda hakujiuzulu hadi mwaka 2000.

Mwezi Machi 1999, Jaji aliamua kwamba Kaunda anyang’anywe uraia wa Zambia kwa sababu wazazi wake walikuwa raia kutoka Malawi na zaidi ya hayo, kwa sababu ya ukweli huo, Kaunda alishika nyadhifa ya urais kinyume cha sheria, kipindi chake chote serikalini.

Kaunda alipata changamoto, lakini uraia wake ulirejeshwa mwaka uliofuata baada ya pingamizi lililokuwa limewekwa dhidi yake kuondolewa kortini.

Mwaka 2002 Kaunda aliteuliwa kuwa Rais Mkazi wa Afrika katika Chuo Kikuu cha Boston, nchini Marekani (Balfour African President-in-Residence at Boston University), nafasi ambayo aliishikiliwa hadi 2004.

Mwaka 2003 Kaunda alipewa Tuzo ya Heshima (Grand Order of the Eagle Zambia) na Rais Levy Mwanawasa aliyechukua madaraka baada ya Chiluba.

Ugonjwa na kuumwa

Juni 14, mwaka huu, Kaunda alilazwa katika Hospitali ya kijeshi ya Maina Soko, Lusaka na kutibiwa ugonjwa ambao haujawekwa wazi.

Serikali ya Zambia ilisema madaktari wanafanya kila jitihada ilia pate nafuu, ingawa haikuwekwa wazi anasumbuliwa na nini. Juni 15, 2021, ilibainishwa kuwa anasumbuliwa na pneumonia na kwa mujibu wa daktari imekuwa ni shida ya mara kwa mara kweny afy yake. Juni 17, mwaka huu ilithibitishwa kuwa amefariki akiwa na umri wa miaka 97 baada ya kuugua kwa muda mfupi katika hospitali ya kijeshi ya Maina Soko.

Rais Edgar Lungu alitangaza katika ukurasa wake wa Facebook kuwa Zambia itakuwa na siku 21 za maombolezo ya kitaifa. Rais Samia Suluhu Hassan 

ametangaza kuwa Tanzania itaomboleza kwa siku saba na Rais wa Botswana, Dk Mokgweetsi Masisi, alitangaza siku saba za maombolezo Botswana.

Hakika Kaunda au KK atakumbukwa na Waafrika na dunia kwa ujumla, kwani alikuwa miongoni mwa viongozi mahiri na jasiri Afrika kutokana na mchango mkubwa kwenye harakati za ukombozi wa Bara la Afrika kwa kushirikiana na viongozi wengine, akiwemo Baba wa Taifa, Julius Nyerere. Lakini pia ni miongoni mwa waanzilishi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Atakumbukwa pia kwa mchango wake katika kukuza uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia ambao uliwezesha kutekelezwa kwa miradi mikubwa ya kimkakati, hususani Mamlaka ya Reli kati ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na Bomba la Kusafirisha Mafuta (TAZAMA).

Hata katika mavazi, Kaunda atakumbukwa kwani alipenda na alijulikana kwa kuvaa ‘safari suit” (jaketi la safari na suruali), mara kwa mara , hadi leo safari suit inajulikana kama “Kaunda 

suit” katika maeneo yote ya Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Vile vile kwa wasiofahamu, Kaunda aliwahi kuandika pia muziki juu ya uhur u ambao alitarajia kuupata, ingawa ni wimbo mmoja tu unaojulikana miongoni mwa raia wa Zambia ambao ni “Tiyende pamodzi ndi mtima umo” kwa maana halisi ni “wacha tutembee pamoja kwa moyo mmoja.”

Mwezi Septemba 2019, Kaunda alisema ni jambo la kusikitisha kwamba Rais Robert Mugabe (marehemu) alipakwa matope na watu kutoka maeneo mengine ulimwengu, ambao walikuwa hawataki aendeshe kampeni ya kuleta haki kwa jamii na usawa Zimbabwe.

Familia

Kaunda alikuwa mkewe Beatrice Kaunda (marehemu) aliyefariki mwaka 2012 na walibarikiwa watoto nane. Lakini pia ameacha wajukuu 30 na vitukuu saba.

Kaunda siku zote atakumbukwa kwa namna alivyowathamini na kuwaheshimu viongozi wenzake na wapigania uhuru katika bara hili la Afrika. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.Amen.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/dca38f278465c62626ca899c741b1064.jpeg

NCHINI Tanzania kuna matajiri wengi wakubwa walioanzia ngazi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi