loader
Dstv Habarileo  Mobile
BancABC yatoa riba asimilia 14 mwanzoni

BancABC yatoa riba asimilia 14 mwanzoni

BENKI ya BancABC Tanzania imetangaza kuzindua kampeni kabambe ya kuweka fedha katika akaunti ya amana kwa wateja wote itakayomwezesha mteja kupata riba ya hadi asilimia 14 kwa mwaka mara tu, anapoweka akiba hiyo.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam Juni 23 wakati akitangaza kampeni hiyo, Mwendeshaji Mkuu wa Biashara wa BancABC-Tanzania, Joyce Malai, amesema benki hiyo imeanzisha utaratibu wa kutoa riba ya hadi asilimia 14 kwa wateja wote wanaofungua akaunti za amana kuanzia jana hadi mwishoni mwa Septemba.

Amesema mteja atalipwa riba hiyo papo hapo huku fedha ikiendelea kusalia kwenye akaunti hadi muda uliokusudiwa wa mwaka mmoja, miezi sita au miezi mitatu uatakapotimia.

“Hii ndio ofa kabambe na bora kwenye soko kwa sasa, tunawahimiza wateja wetu na pia kwa wale ambao si wateja wetu, kuchangamkia fursa hii na kuwekeza kwenye akaunti ya amana ya BancABC kabla muda wa ofa hii haujaisha,” amesema.

Malai amesema BancABC imedhamiria kuendelea kutimiza mahitaji ya wateja wake kwa kuhakikisha kuwa wote wanafaidika na wanakuwa kwa pamoja.

“Tunatoa riba papo hapo ili kufanya wateja wetu waendelee kuendesha biashara zao pamoja na shughuli zao za kila siku bila kusubiri muda uliokusudiwa wa akaunti ya amana ufike ndio wapate fedha zao.”

“Hili la BancABC kutoa malipo ya riba mwanzoni ni jibu la ombi lililotolewa na wateja ikiwa ni hatua ya kufaidi mapema pato au mavuno yanayotokana na uwezekezaji wao kwa kipindi hicho.”

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a186f6804eddcabfa85c80cef313449b.JPG

MKURUGENZI wa Idara ya Diplomasia ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi