loader
Masoko haya yatunzwe yabaki masafi

Masoko haya yatunzwe yabaki masafi

SERIKALI imeendelea na kasi ya uboreshaji wa biashara hapa nchini kwa kujenga masoko ya kisasa yatakayokidhi mahitaji ya wananchi.

Miongoni mwa masoko ya kisasa yaliyojengwa hivi karibuni ni soko la Kisutu na lile la Magomeni huku kukiwa na matarajio ya kujenga masoko ya kisasa zaidi hasa katika jiji la Kibiashara la Dar es Salaam.

Mpango wa serikali una nafasi kubwa zaidi kuhakikisha wakulima na wafanyabishara wanakuwa katika mazingira mazuri huku wateja wakipata huduma zao katika hali ya unadhifu zaidi.

Masoko hayo ya kisasa yamekuwa na ulinzi na maeneo ya kuegesha magari kwa ajili ya wateja wanaofika hapo hivyo kuwa na uhakika na huduma nzuri Mwezi huu wa Juni,2021 soko la kisasa la Kisutu limeanza kufanya kazi huku tayari wafanyabiashara 463 wakiwa wameshahamia na wengine wanataraijia kuhamia hivi karibuni.

Soko hilo ambalo limejengwa kwa fedha za serikali zenye thamani ya Sh bilioni 16 lenye ghorofa nne linatarajia kuchukua jumla ya wafanyabiashara 1,500 Ukisasa wa soko hilo ni uwepo wa sehemu za kutoa huduma mbalimbali kama za kumbi,huduma za kibenki ofisi,vizimba na vioski au tuseme fremu.

Pamoja na uzuri wa soko na huduma zake iko haja ya wahusika kuhakikisha kwamba tabia inajengeka ya watu kujali unadhifu wa masoko hayo kila upande kwanza kwa kufanya pawe mahali pa kuvutia na pili kuweza kuepusha magonjwa ya mlipuko yanayosababishwa na uchafu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/48a1adbe43292849625124ef90065bbb.jpg

MOJA ya misemo maarufu ya Rais mstaafu Ali Hassan ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi