loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Kiir awapandisha  vyeo wanajeshi 3,000

Rais Kiir awapandisha vyeo wanajeshi 3,000

RAIS Salva Kiir  amewapandisha vyeo wanajeshi zaidi ya 3,000  ili kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wananchi.

Msemaji wa Polisi, Meja Jenerali Daniel Boulo alisema  mwishoni mwa wiki kuwa, Rais Kiir amewapandisha vyeo maofisa 22 wa polisi kutoka cheo cha Brigedia Jenerali kuwa  Meja Jenerali, huku wengine wakipandishwa kutoka cheo cha Kanali  kuwa  Brigedia na Brigedia Jenerali.

Alisema maofisa waliopandishwa vyeo wanatoka katika majimbo 10 yaliyoanzishwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya kuwa kwenye orodha ya kusubiri kupandishwa vyeo tangu mwaka 2017.

“Tunatakiwa kuwapandisha vyeo wafanyakazi  wetu kila mwaka. Pendekezo la kuwapandisha vyeo hawa  lilitolewa mwaka 2017 na 2018."

“Kuna kamati iliundwa kwa ajili ya kusimamia jambo hili na majimbo yote yalitakiwa kutoa ripoti kuhusu wafanyakazi na kuwasilisha kwa kamati hiyo pamoja na mapendekezo kwa viongozi wa jeshi na baadaye kwenda kwa Rais ambaye amewapandishwa vyeo walitangazwa,” alisema Jenerali Justin.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/95e3801e75712c49c4f43b173cb57497.jpeg

Katika hali isiyo ya kawaida, Mwanaume mmoja amekutana ...

foto
Mwandishi: JUBA 

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi