loader
Dstv Habarileo  Mobile
EU sasa kuiondolea   vikwazo Burundi

EU sasa kuiondolea  vikwazo Burundi

UMOJA wa Ulaya (EU) umeanza mchakato wa kuondoa vikwazo kwa Burundi.

Umoja huo uliiwekea Burundi vikwazo mwaka  2015 wakati wa machafuko ya kisiasa baada ya Rais wa zamani, Rais Pierre Nkurunziza kuongeza muda wa kuongoza na kusababisha maandamano.

Balozi wa EU nchini Burundi, Claude Bochu aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa, mwisho wa Mei mwaka huu, vikosi kazi vya EU viliamua kwa kauli moja taasisi za Mahakama za umoja huo kubatilisha kusimamishwa kwa msaada wa kifedha kwa serikali ya Burundi.

Alisema hatua hiyo ilifikiwa baada ya kufanya mkutano na Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye na kuona  maendeleo makubwa chini ya utawala wake katika kukuza utawala wa sheria na haki za binadamu.

Alisema EU inatarajia matokeo mazuri zaidi na kuwa pamoja na washirika wengine kama Benki ya Maendeleo ya Afrika watagharamia ukarabati wa Bandari ya Bujumbura na maeneo yake ya karibu kabla ya mwisho wa mwaka huu na kuchangia fedha katika  sekta ya kilimo.

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hivi karibuni ilitoa  mwito kwa EU kuondoa vikwazo kwa Burundi, ikisema nchi hiyo  iko tayari kusonga mbele.

Katibu Mkuu wa EAC, Peter Mathuki alisema vikwazo hivyo vinawaumiza wananchi wa Burundi pamoja na watu wote wa ukanda wa Afrika Mashariki.

EAC inajumuisha nchi sita za  Burundi, Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Sudan Kusini. 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7e81083e0b9285e8bfafe4b3d5e2dcfe.png

Katika hali isiyo ya kawaida, Mwanaume mmoja amekutana ...

foto
Mwandishi: BUJUMBURA

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi