loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kampuni 13 za Tanzania zawekeza Rwanda

Kampuni 13 za Tanzania zawekeza Rwanda

KAMPUNI zaidi ya 13 za Tanzania zimewekeza nchini Rwanda katika sekta mbalimbali ikiwamo usafi rishaji, uzalishaji wa bidhaa, biashara za mafuta ya magari na mitambo pamoja na utoaji huduma za aina mbalimbali.

Akizungumza na HabariLEO, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Ernest Mangu aliliambia HabariLEO alitoa mwito kwa Watanzania kwenda kuwekeza zaidi na kuchangamkia fursa mbalimbali za biashara nchini humo kutokana na uhusiano uliopo baina Tanzania na Rwanda.

“Watanzania wajipange kunufaika na hali nzuri ya uhusiano iliyopo baina ya nchi zetu kwa kutafuta fursa za biashara zilizopo ikiwamo kuuza bidhaa zenye soko kubwa Rwanda ikiwamo mahindi, mihogo, mchele, karanga, tangawizi, saruji, makaa ya mawe, vinywaji baridi na pombe aina ya konyagi na nyinginezo.

Mangu alisema hali mpakani iko vizuri kwa mizigo kuingia na kutoka bila shida ingawa kwa sasa imefungwa kwa biashara za kawaida kama hatua ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Aidha, alisema anavutiwa na Rwanda kwa nidhamu ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali kwa watendaji wa umma kuwa na uwajibikaji.

Alisema kutokana na kuendelea kuimarika kwa uhusiano baina ya nchi hizo, Watanzania wanatakiwa kuingia nchini humo kuwekeza na kufanyabiashara mbalimbali na kama watakumbana na changamoto zozote watoe taarifa ili ziweze kushughulikia kidiplomasia.

“Rwanda ni mshirika wa biashara na Tanzania, kuna wafanyabiashara wakubwa wa Rwanda wanatumia Bandari ya Dar es Salaam kusafirisha mizigo yao na wengine wakinunua bidhaa mbalimbali nchini na kuuza Rwanda,” alisema.

Tanzania na Rwanda zinategemeana kwa kiwango kikubwa kwa takribani asilimia 70 ya bidhaa zinazotoka na kuingia Rwanda zinapitia kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

Takwimu za mwaka 2018 zinaonesha Tanzania imekuwa ikiuza bidhaa mbalimbali nchi Rwanda zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 685.63 kwa mujibu wa Takwimu za biashara za kimataifa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (Comtrade) zilizofanyiwa marekebisho kwa mara ya mwisho Mei, mwaka huu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/01d3a333bb3b6e44b720699a7db4494f.jpg

MKURUGENZI wa Idara ya Diplomasia ya ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi