loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kila mmoja ashiriki kufanikisha Mpango wa Maendeleo ya Taifa

Kila mmoja ashiriki kufanikisha Mpango wa Maendeleo ya Taifa

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa jana alizindua Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/2022–2025/2026 utakaogharimu Sh trilioni 114.8, ambao sekta binafsi inatarajiwa kuchangia Sh trilioni 40.6 na sekta ya umma Sh trilioni 74.2.

Amesema serikali itahakikisha malengo ya mpango huo yanafikiwa na kamwe hawatafumbia macho tabia ya ukwepaji kodi, uzembe kazini, ufujaji wa fedha na rushwa na kuendelea kuenzi bunifu na kupokea mawazo mbadala yenye lengo la kuboresha utekelezaji wa mpango huo.

Huu ni mpango ambao umetumika katika kuhakikisha nchi inaweka vipaumbele vyake ambavyo kutokana na mpango huo wa miaka mitano, vipaumbele hivyo huwekwa katika utekelezaji wa mwaka mmoja mmoja ambao hutumika katika kuandaa bajeti ya serikali kwa kila mwaka husika.

Ndio mpango ambao unaelekeza nini cha kufanywa na serikali na mara zote umeanisha kama alivyoeleza Waziri Mkuu, mipango ya kusimamiwa na serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi katika kuhakikisha mipango na vipaumbele vinafikiwa na hivyo kuwaletea Watanzania maendeleo yaliyokusudiwa.

Ni kwa msingi huo, Mpango wa Maendeleo ya Taifa ni muhimu mno na ushiriki wa kila mmoja katika kufanikisha mpango huu unahitajika, hivyo tuna amini kila Mtanzania atatoa mchango wake kufanikisha malengo yaliyoainishwa katika mpango huu wa miaka mitano.

Tuna amini sekta binafsi pamoja na washirika wa maendeleo ambao wote ni wadau muhimu katika kufanikisha mpango huu, watashiriki kikamilifu kwa kuchangia fedha walizoahidi katika kuhakikisha zinapatikana ile ziende kuendeleza na kukamilisha miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa sasa nchini pamoja na mipya iliyopangwa katika mpango huo.

Hatutarajii kwa wasimamizi wa mpango huo wakiwemo watendaji wa serikali watakuwa kikwazo katika utekelezaji ama kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu au kwa kushiriki katika vitendo viovu kama rushwa, uzembe kazini na ufujaji wa fedha zilizopangwa kuutekeleza.

Tumeona juhudi kubwa zilizofanywa na zinazofanywa na serikali kuboresha maisha ya Watanzania, hivyo tuna amini hatatokea mtu wa kukwamisha juhudi hizo kupitia mpango huu uliozinduliwa jana.

Ni vyema kila mmoja akatimiza wajibu wake ili kuhakikisha kaulimbiu ya Rais Samia Suluhu Hassan ya ‘Kazi Iendelee,’ inaendelea kwa kasi kubwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/cab054a00cf532b5fe38e06c568b3cf7.jpg

KWA mara ya kwanza leo dunia inaadhimisha ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi