loader
Dstv Habarileo Mobile
Veta yaleta mashine kufukuza ndege shambani

Veta yaleta mashine kufukuza ndege shambani

MAMLAKA ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) imesikia kilio cha wakulima wa mpunga, mtama, ulezi, ufuta na alizeti wanaosumbuliwa na ndege kwa kuwatengenezea mashine ya kufukuza ndege waharibifu wa mazao inayotumia umeme wa jua.

Kutokana na utalaamau huo, wakulima katika maeneo yanayosumbuliwa na ndege hao waharibifu wa mazao wakiwamo kweleakwelea na wengineo, sasa hawana haja kuhatarisha afya zao kwa kufunga medebe na mabati chakavu kama njia ya kuwafukuza ndege hao.

Mwalimu wa Veta kutoka Mikumi mkoani Morogoro ambaye ni mtaalamu wa umeme na vifaa vya umeme, Jones Hokororo, aliliambia HabariLEO kuwa, mashine hiyo iliyotengenezwa kwa kutumia chuma kigumu hata ikiwekwa katika jua au mvua haiwezi kuathiriwa.

Alisema mashine hiyo imewekewa sauti za ndege wakubwa maadui wa ndege waharifu kama tai na mwewe ambao chakula chao ni kweleakwelea.

Alisema kwa kuwa ndege waharibifu wanaogopa zaidi maadui kama tai na mwewe, wakisikiapo sauti za ndege hao wakubwa ambao ni maadui  na hatari kwao,  hukimbilia mbali na kujificha wakiogopa kuliwa.

Mtaalamu huyo alisema mkulima anapobonyeza kitufe cha mashine hiyo inayotumia umeme jua, hutoa mlio wa ndege hao wakubwa na hatari kwa ndege waharibifu kwa takriban  sekunde 18 kisha kupumzika na kuwaka tena baada ya dakika tano.

"Huu ni masada mkubwa kwa wakulima kwa kuwa mashine hiyo ina spika zinazoota sauti kali inayosikika kwa umbali hata wa mita zaidi ya mia moja," alisema.

Kwa mujibu wa Hokororo, mashine hiyo inayo9weza pia kuendeshwa kwa kutumia simu za mikononi kwa kutumia programu ya ‘bluetooth’ umbali wa mita 20, inauzwa Sh150,000 bei ambayo kila mkulima wa Tanzania anaimudu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/fda8ea776b15e48ff62da8b6fdbe0cb3.jpeg

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha na Selemani Nzaro

2 Comments

 • avatar
  Bernard
  02/07/2021

  ubunifu mzuri hongera

 • avatar
  Kyaro
  03/07/2021

  Tunaomba mnapotoa matangazo kama haya muweke contacts zenu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi