loader
Dstv Habarileo  Mobile
Huawei, ATU  zakubaliana kujengea uwezo nchi za Afrika katika mabadiliko ya Tehama

Huawei, ATU zakubaliana kujengea uwezo nchi za Afrika katika mabadiliko ya Tehama

JUMUIYA ya Mawasiliano ya Afrika (ATU) imetia saini Mkataba wa Makubaliano na Kampuni ya teknolojia ya Huawei ambayo itahakikisha nchi na mashirika ya kiafrika yanajenga uwezo kwa ajili ya mabadiliko ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Katika makubaliano hayo, Huawei itatoa mafunzo ya kukuza ujuzi wa kidijiti na kuhakikisha mashirika hayo mawili yanashirikiana kusaidia ubunifu wa ndani, kubadilishana habari juu ya mwenendo wa mambo, changamoto na suluhisho kwa Afrika na ulimwenguni huku ikipanua uchumi wa kidijiti pamoja na unganisho la vijiji kupitia utafiti.
Hatua hiyo inakuja huku ripoti ya mwaka 2019 ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo (UNCTAD) juu ya uchumi wa kidijiti ikionesha kuwa Afrika na Amerika ya Kusin kwa pamoja zinachangia chini ya asilimia tano ya vituo vya data ulimwenguni.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ni kwamba ikiwa suala hilo litaachwa bila kushughulikiwa, kutakuwa na ongezeko katika mgawanyiko wa usawa wa mapato uliopo sasa. Hii, ikijumuishwa na ukweli kwamba katika nchi zinazoendelea, ni mtu mmoja tu kati ya watano anayetumia intaneti ikilinganishwa na watu wanne kati ya watano katika nchi zilizoendelea.
Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini iliyofanyika hivi karibuni jijini Nairobi, Kenya, katika makao makuu ya ATU, , Katibu Mkuu wa ATU John Omo, aliipongeza Kampuni ya Huawei kwa mchango wake barani Afrika.
"Huawei imebadilisha muunganiko na imetoa mchango mkubwa barani Afrika  kupitia uwekezaji wake katika miundo mbinu ya kidijiti ambayo ni rafiki kwa mazingira, kutoa ufundi wa ICT pamoja na teknolojia za hali ya juu kwa maeneo ya vijijini. Shirika hili ni mshirika wa maendeleo anayeaminika barani Afrika. Makubaliano haya tunayosaini yanalenga kuimarisha ushirikiano huu," alisema.
Aliongeza kuwa Afrika ina nafasi kubwa ya kunufaika kutokana na teknolojia mpya.
Mashirika hayo mawili yana historia ya muda mrefu ya kufanya kazi pamoja na makubaliano hayo mapya yatasaidia nchi za kiafrika, wasimamizi na wananchi kufaidika na mabadiliko ya uchumi wa kidijiti, kuhamia kwa teknolojia mpya, kukuza mitandao salama na kupata ujuzi wa kidijiti unaohitajika ili kusukuma uchumi mbele.
Makamu wa Rais wa Huawei Kusini mwa Afrika, Samuel Chen aliishukuru ATU kwa uongozi na uendelezaji wa Tehama barani Afrika: "ATU inachukua jukumu muhimu kusaidia nchi wanachama katika sera na mikakati yao, kusaidiana uzoefu, kujenga uwezo na kuendesha ubunifu na tunafurahi kuweza kuwaunga mkono...
"...Tumeunganisha mamilioni ya Waafrika katika huduma salama, za kasi na za mtandaoni katika kipindi cha miongo miwili iliyopita na kupata uaminifu na msaada wa wateja wetu na wasimamizi.Tunatarajia kufanya hata zaidi”.
Kulingana na makubaliano hayo, washirika wataanza kutoa mafunzo kwa ATU ambao watapata nafasi ya kushirikiana na wataalamu kutoka kote ulimwenguni kujadili teknolojia na mwenendo wa mambo pamoja na kushirikiana kwenye utafiti kusaidia maendeleo ya kidijiti barani Afrika.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/b03d3112f4227fc5a8c37eeca09db3cf.jpg

Katika hali isiyo ya kawaida, Mwanaume mmoja amekutana ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi