loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kazi iendelee uboreshaji usalama barabarani

Kazi iendelee uboreshaji usalama barabarani

SEKTA ya barabara ni kati ya ambazo zimebeba hatma ya maendeleo ya  nchi kiuchumi, kijamii na hata kisiasa.

Barabara zimekuwa zikitumika kusafirisha bidhaa mbalimbali pamoja na watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine . Kwa lugha rahisi, sekta ya barabara imebeba roho ya uchumi kwa nchi na pia ustawi wa watu.

Hivyo usalama wa barabara ni jambo muhimu linalopaswa kuzingatiwa na serikali pamoja na wadau mbalimbali kwa kuzingatia sheria zilizowekwa.

Sheria ya usalama barabarani ni mwongozo mzima unaotakiwa kufuatwa katika matumizi bora . Inamaanisha sheria inayowabana watumiaji wa barabara, vyombo vya usafiri, wasimamizi wa masuala ya usalama barabarani na mengineo mengi.

Kwa sasa Sheria ya Usalama Barabarani inayotumika ni ya mwaka 1973 ambayo hakika imepitwa na wakati kutokana na mabadiliko ya mambo mengi katika matumizi ya huduma ya barabara ikilinganishwa na ilivyokuwa miaka hiyo ilipotungwa.

Ili kuendana na kauli mbiu ya Rais Samia Suluhu Hassan ya ‘Kazi Iendelee’, kunahitajika sheria mpya ya usalama barabarani itakayokidhi matakwa ya mabadiliko ya sasa.

Mfano Sheria ya Usalama Barabarani ya mwaka 1973 imemtaja mwendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kuwa anapaswa kuvaa kofia ngumu.

Na hiyo inatokana na ukweli kuwa kwa miaka hiyo, pikipiki hazikuwa zikitumika kama chombo cha usafiri kibiashara tofauti na sasa ambapo pikipiki zinabeba abiria hivyo uvaaji wa kofia ngumu ni lazima kwa abiria na dereva.

Nionavyo, ili kuboresha matumizi bora ya barabara yawe salama ni lazima sheria kuboreshwa.

Napongeza hatua ya awali ya Bunge ya kupokea muswada ya sheria hiyo ya mwaka 1973 ambao kati ya mambo yalioangaziwa ni pamoja na kudhibiti mwendokasi, kuhakikisha matumizi bora ya vizuizi vya watoto vinatumika wakati wa safari, kiwango cha pombe, ufungaji wa mikanda na uvaaji wa kosia ngumu.

Mambo haya na mengine mengi yaliyomo kwenye muswada, yakitungiwa sheria, kutakuwa na matumizi bora ya barabara yatakayochagiza maendeleo ya uchumi na kazi kuendelea.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/badb22817eebde42f7753e7a95482e55.jpg

TAARIFA za matukio ya mimba na ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi