loader
Dstv Habarileo  Mobile
Polisi aliyekuwa akisakwa  kwa mauaji akutwa amekufa

Polisi aliyekuwa akisakwa kwa mauaji akutwa amekufa

OFISA mmoja wa polisi ambaye amekuwa mafichoni baada ya kuwaua watu wawili amepatikana akiwa amefariki dunia.

Mwili wa polisi huyo, Caroline Kagongo ambaye alikuwa akisakwa baada ya kuwaua watu wawili, umepatikana nyumbani kwa wazazi wake kaunti ya Elgeyo Marakwet eneo la Rift Valley.

Kwa mujibu wa Polisi, askari huyo alimuua kwa kumpiga risasi mwenzake, John Ogweno Julai 5, mwaka huu na kutorokea eneo la Juja jijini Nairobi na kisha kumuua mtu mwingine aliyetambuliwa kwa jina la  Peter Ndwiga kwa kumpiga risasi katika chumba cha hoteli.

Vyombo vya habari nchini Kenya vilimnukuu Kamishna wa Polisi Kanda ya Rift Valley, George Natembeya akithibitisha tukio hilo.

Habari zinasema Kagongo alijiua kwa kujipiga risasi kwa kutumia bastola ambayo anatuhumiwa kuitumia kutekeleza mauaji hapo awali.

Mwili wake ulipatikana bafuni majira ya 1:30 asubuhi.

Polisi walipata wakati mgumu kujua aliko kwa sababu aliiacha simu yake katika eneo la kwanza alikotekeleza mauaji .

Mkurugenzi wa Idara ya Jinai, George Kinoti alitoa wito kwa umma kusaidia Polisi kumkamata polisi huyo ambaye alimuelezea kuwa sugu, aliyejihami na hatari.

Kangogo alihudumu katika vituo mbalimbali vya polisi ikiwamo kitengo reli kabla ya kupelekwa Nakuru ambako amefanya kazi kwa karibu miaka mitatu.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/a0f3923bae0ee5e2ce488ec90312f4be.jpg

Katika hali isiyo ya kawaida, Mwanaume mmoja amekutana ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi