loader
Dstv Habarileo  Mobile
70 wakodisha ndege kuhudhuria kongamano la Samia Burundi

70 wakodisha ndege kuhudhuria kongamano la Samia Burundi

WAFANYABIASHARA 70 wa Tanzania wamekodisha ndege ya Shirika la Ndege (ATCL) kwenda Burundi kushiriki kongamano la biashara lililohudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake, Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana kabla ya kuondoka, Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula alisema wameamua kwenda kwa wingi nchini Burundi kutokana na umuhimu wa kongamano hilo.

“Wafanyabiashara kwa umoja wetu tumeamua kwenda kumuunga mkono Rais Samia kwa jitihada zake za kuimarisha uchumi wa nchi hii kupitia sekta ya biashara. Burundi kuna fursa lukuki ambazo tumeona ni wakati wetu wa kunufaika nazo,” alisema Ngalula.

Alisema Burundi kuna fursa nyingi za biashara ambazo wafanyabiashara wa Tanzania wanatakiwa kuzitumia katika kukuza uchumi.

Alisema wafanyabiashara wamejipanga kutumia fursa hizo ipasavyo ili kukuza uchumi wao na wa nchi na kwamba TPSF imeguswa na namna ambavyo Rais Samia amekuwa akinadi na kufungua milango ya biashara ya Tanzania kwa mataifa mengine.

Mfanyabiashara, Mustapha Hassanali alisema hatua ya Rais Samia kwenda nchini humo kufanya ziara, itadumisha udugu kati ya Tanzania na Burundi na hivyo kufungua zaidi milango ya uchumi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/bbaad4fe475d495b46b9e88e44e88d26.png

Katika hali isiyo ya kawaida, Mwanaume mmoja amekutana ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi