loader
Dstv Habarileo  Mobile
Bocco, Gomes wang’ara tuzo za Ligi

Bocco, Gomes wang’ara tuzo za Ligi

KOCHA Mkuu wa klabu ya Simba, Didier Gomes, ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi Juni baada ya kuisaidia timu yake kumaliza ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi, huku nahodha wake John Bocco, pia akiibuka kuwa mchezaji bora.

Mwingine aliyechukua tuzo ya mwezi Juni ni Meneja wa Uwanja wa CCM Kirumba, Jonathan Mkumba, hii inakuwa tuzo ya pili kwa kocha huyo ambaye alitwaa tuzo ya kwanza Aprili mwaka huu naye mshambuliaji John Bocco, amechukua tuzo hii ya mchezaji bora kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo Novemba, 2020.

Akizungumza jana, Gomes alisema kuwa ni jambo la faraja  kutwaa tuzo hii kwani inampa motisha ya kufanya vizuri zaidi  katika kazi yake kama kocha  akiwa mwishoni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara itakayofika tamati kesho na Kombe la Shirikisho la Azam, ambalo fainali yake itachezwa Julai 25.

“Tuzo hii ni heshima kwangu pamoja na wachezaji wangu ambao nafanya nao kazi inatufanya tuendelee kupambana kwaajili ya Simba ili kutimiza malengo yetu tuliyojiwekea msimu huu,” alisema Gomes.

Naye nahodha John Bocco, alisema kuwa sio jambo rahisi kutwaa tuzo hii kutokana na ubora wa wachezaji waliopo katika ligi kushinda kwake kuna mfanya azidi kukaza mkanda zaidi katika mchezo uliyosalia ili aweze kutwaa kiatu cha ufungaji bora.

“Tangu nimekuja hapa sijawahi kutwaa kiatu cha dhahabu naamini huu ni msimu wangu wa kufanya hivyo kama nitapata nafasi katika mchezo uliosalia,” alisema Bocco.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/ed0117b933775e246c380180a4ff58c8.jpg

AISHI Salum Manula sio jina geni ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi