loader
Dstv Habarileo  Mobile
DK Mwinyi ataka kalenda Zanzibar Marathoni

DK Mwinyi ataka kalenda Zanzibar Marathoni

RAIS wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi,  ameishauri  Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale  kuandaa kalenda maalum ya Mashindano ya Kimataifa ya  Marathoni  (Zanzibar International Marathon ), ili kuwawezesha wadau kuzitangaza mbio hizo katika maonesho ya kimataifa ya Biashara na Utalii, yanayofanyika kila mwaka.

Dk. Mwinyi ametoa ushauri huo jana katika Uwanja wa Amani jijini Zanzibar kwenye Mashindano ya Kimataifa ya Marathon 2021 zilizoanzia Forodhani na kuwashirikisha wanariadha kutoka ndani na nje ya Zanzibar na wananchi kwa ujumla.

Kalenda hiyo itaendana na madhumuni ya msingi ya kurudishwa mbio hizo na kuitumia njia hiyo kama moja ya vivutio vya kukuza sekta ya utalii, kuongeza ajira kwa vijana pamoja na kukuza uchumi wa Taifa. 

Alisema Serikali itatoa ushirikiano katika kuendeleza michezo mbali mbali  na kuhakikisha mbio za kimataifa za Marathoni  zinafanyika kila mwaka ikiwa ni  hatua ya kutoa wanariadha wenye vipaji na uwezo  wa kushindana Kimataifa.

 “Nimefarijika sana tumeweza kuzirudisha tena mbio hizi zilizositishwa kuandaliwa na hatimae kutoweka kabisa kwa zaidi ya miaka kumi sasa,” alisema.

Dk. Mwinyi alisema Serikali ya awamu ya nane inahamasisha ubunifu na kuandaa mazingira mazuri zaidi ya kisera na kisheria, ili kurahisisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo.

Alisema katika kuimarisha sekta ya utalii, Serikali imejipanga kuimarisha miundombinu mbalimbali ya michezo kwa kiwango cha kimataifa ili michezo hiyo  iwe sehemu ya kukuza utalii.

Pia alisema serikali ina azma ya kufufua mashindano ya Triathlon yanayojumuisha michezo ya kuogelea, mbio za baiskeli na kukimbia, ili kuongeza idadi ya watalii  nchini.

Rais Dk. Mwinyi ambaye alikuwa miongoni mwa washiriki wa mbio hizo za kilomita tano alitumia fursa hiyo kuwahimiza wafanyabiashara na wawekezaji kujitokeza kudhamini timu na klabu za michezo  kwani hatua hiyo itaamsha ari na hamasa ya wanamichezo na mashabiki.

Aidha, Rais wa Chama cha Riadha Zanzibar, alitumia fursa hiyo kumuomba Rais Mwinyi kuwa mlezi wa chama cha Riadha Zanzibar.

Mashindano ya Kimataifa ya  Marathon (ZIM 2021) yaliokuwa katika masafa ya Kilomita 21, 10 na 5  na mbio za nyongeza za kilomita 400 na  mbio za watoto na watu wenye ulemavu, yaliwashirikisha wanariadha  2000 kutoka Tanzania, Kenya, Rwanda, Afrika Kusini, Ufaransa, Switzerland na wenyeji Zanzibar.

Katika mashindano hayo ya kilomita 21 mshindi wa kiume alikuwa ni Panel Mkumbo na wa kike alikuwa  Pamela Chepkoech wote kutoka Kenya.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/b6ca6562f942e67ff0c12f36e4dc7f45.jpg

AISHI Salum Manula sio jina geni ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi