loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mfuko wa Dunia watoa dola milioni 53 kukabili malaria

Mfuko wa Dunia watoa dola milioni 53 kukabili malaria

SERIKALI imepokea ruzuku ya dola za Marekani milioni 53 kutoka Mfuko wa Dunia (Global Fund), ikiwa ni sehemu ya dola milioni 280 zinazohitajika katika kuzuia na matibabu ya ugonjwa wa malaria kuanzia mwaka 2020 mpaka 2024.

Hadi kufikia Septemba, mwaka jana, serikali ilikuwa imepokea ahadi kutoka vyanzo mbalimbali ya ya takribani asilimia 74 ya fedha hizo, lakini ilikuwa ikitafuta dola za Marekani milioni 73 kukamilisha  mpango huo ambao unakusudia kuongeza kasi ya kumaliza malaria nchini.

Mkuu wa Kitengo cha Maambukizi ya Malaria na Kitengo cha Maambukizi ya Vimelea katika Kituo cha Biomedical cha Rwanda, Dk Aimable Mbituyumuremyi alisema kuanzia mwezi huu, Mfuko wa Dunia utaanza kutoa fedha za miaka mitatu ijayo kwa kulenga maeneo maalumu.

Alisema fedha hizo zitakuwa na matokeo mazuri katika kupunguza  idadi ya vifo na maambukizo ya malaria.

"Fedha hizo zitatumika kupuliza dawa katika wilaya sita kwa miaka mitatu ijayo, ununuzi wa vyandarua vyenye dawa na ununuzi wa bidhaa za malaria ikiwamo vifaa vya kupima malaria, dawa za malaria na kusaidia wafanyakazi wa afya ya jamii," alisema.

Rwanda pia ilipokea ufadhili kutoka Marekani kupitia  Mpango wa Rais wa Kudhibiti Malaria (PMI) kiasi cha dola za Marekani milioni 18 na zitatumika kunyunyiza dawa za kuua vimelea vya malaria katika wilaya tatu ununuzi wa vyandarua na dawa za malaria. 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/03ef7454785c641e952a800edd0652a6.jpeg

SERIKALI imetangaza kuwa watumishi wa umma kuanzia mwaka ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi